Mtatiro: Wakati tunafurahia babu Seya na mwanaume kuachiwa tusijisahulishe kuwa wako mashaikh Gerezani. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 December 2017

Mtatiro: Wakati tunafurahia babu Seya na mwanaume kuachiwa tusijisahulishe kuwa wako mashaikh Gerezani.

 
 Wakati tunafurahia Babu Seya na mwanaye kuachiwa kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais (Hata mimi nimefurahi). Tusijisahaulishe kuwa wapo Masheikh kadhaa wa taasisi ya UAMSHO ya Zanzibar ambao hadi leo wanashikiliwa gerezani Dar Es Salaam bila kushtakiwa kwa makosa yoyote (wako kizuizini)!

Tusijisahaulishe pia kuwa hizi busara zilizomtoa Seya Gerezani ndizo zinahitajika katika kufumbua kitendawili cha Maiti zinazookotwa baharini kila siku, kupigwa risasi kwa Lissu, Kupotea kwa Ben Saanane, Kupotea kwa Azory wa MCL na kupotea kwa viongozi wengi wa CUF ambao wamewahi kuchukuliwa pale Rufiji na hadi leo hawajulikani walipo.

Wakati tunamsifia JPM kwa kutekeleza jukumu lake la kikatiba na (huenda) kumtendea haki SEYA, tuendelee kumuhoji JPM juu ya usalama wa wakosoaji wa serikali yake, wenye mawazo tofauti naye na serikali yake, Uhuru wa Bunge na Mahakama, Haki ya vyama vya siasa kufanya shughuli zake, Mustakabali wa Katiba Mpya na kukenga taifa linalojiendesha kwa uwazi na bila visasi.

JPM ndiye Rais wetu, usalama wetu na mustakabali wa nchi yetu vimewekwa chini yake, tuone kuwa kumuhoji na kuihoji serikali yake ambayo ni yetu, ni jukumu letu la kikatiba. Na tukumbuke kuwa yale anayoyatenda siyo HISANI kwetu, wala siyo kwa matakwa yake, ni matakwa ya katiba na utekelezaji wa kiapo cha RAIS. Ni matakwa ya makusanyo ya kodi zetu na rasilimali zetu.

Mimi ntaendelea kumuunga mkono Rais wetu kwakuendelea kuhoji yale ambayo wengi wetu tunaona ni HISANI na yale tunayodhani ni maajabu.

No comments:

Post a Comment

Popular