Mama Anna Mghwira amesema alikuwa kwenye chama tena mwenyekiti lakini anapenda jinsi chama cha Mapinduzi wanavyopanga mambo yao, yanavyoeleweka ndani ya wanachama na mbele ya umma kwa ujumla.
Amesema akiwa kama mkuu wa mkoa Kilimanjaro anashirikiana na vyama vyote ikiwemo CCM, CHADEMA na NCCR ambavyo ndivyo vyama vikubwa mkoani kwake lakini katika vyama vyote, ameona CCM inayobadilika japo anaona juhudi za kila mtu lakini juhudi za mtu anaebadilika huwa ziko tofauti, amesema mtu akiokoka haami duniani bali anatoa taarifa kuwa amebadilika na anataka kuwa mtu bora zaidi.
Anna Mghwira amesema anaiona CCM inayoanza kukataa Rushwa, inayotanguliza maslahi ya Taifa mbele na chini ya uongozi wa Jemedari mahiri, Dkt John Magufuli hadhani kama kuna mtu atapenda kubaki kwani amerudisha hadhi na heshima ilikuyokuwepo ndani ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Amesema baada ya kufanya kazi chini ya serikali kwa takribani miezi sita ameona ana sababu ya kutangaza anapenda kuungana na chama cha Mapinduzi. Amesema kina mama wana jukumu la kubeba maisha ya watu na sura ya Taifa.
Mama Anna Mghwira amesema anaungana na kina mama wenzake wanaotaka kubadilika, kupambana na kutoa muda wao wa thamani kuhakikisha Taifa linakuwa mahali salama pa kuishi na linakuwa mfano wa kulea jamii kiutu, kizalendo na kiuajibikaji.

No comments:
Post a Comment