Jerry Murro: Mimi ni sawa na wabunge kumi wa chadema. - KULUNZI FIKRA

Friday, 8 December 2017

Jerry Murro: Mimi ni sawa na wabunge kumi wa chadema.

Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Jerry Murro amesema kutokana na uwezo wake katika mambo mbali mbali anaweza kujilinganisha na wabunge kumi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mahojiano na kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Jerry amesema kutokana na uwezo wake suala la ubunge kwake ni jambo rahisi tu sawa na kubofya button.

“Mimi Jerry Murro mmoja ni sawa na wabunge 10 wa Chadema, nimewazidi kifikra, kinguvu, kipesa, maadili, kihoja na mambo mengine mengi sana” amesema Jerry Murro.

Katika hatua nyingine Jerry Murro amesema mwaka 2020 si ajabu kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa wakirejea katika Chama cha Mapinduzi (CCM).

No comments:

Post a Comment

Popular