Kubenea akanusha kujivua uanachama wa chadema. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 6 December 2017

Kubenea akanusha kujivua uanachama wa chadema.

 
 Mbunge wa Ubungo, Mhe Saed Kebenea(CHADEMA) amekanusha tetesi kuwa yuko kwenye mpango wa kuhamia CCM. Amesema kinachoenezwa sasahivi ni propaganda ili kukitoa chama chake kwenye ajenda ya kuhoji mambo ya msingi.

“Sijawahi kumweleza mtu kwamba nina mpango wa kuhama CHADEMA, wala sifikirii, sijawahi kukaa na CCM na hayo mambo nayaona kwenye mitandao, kama kuna mtu ana ushahidi wa mimi kuzungumza na CCM autoe, sina sababu za kuhama, imani niliyopewa na Ubungo ni kubwa, siwezi kuichezea,” amesema Mhe Kubenea.

"Kama nikutaka kuondoka CHADEMA nitaondoka kwa hiyari yangu na sio kwa kununuliwa na CCM. Nimejenga jina langu kwa miaka zaidi ya 15. Siwezi kuwasaliti wananchi wa Ubungo" amesema Mhe Kubenea.

"Kuna watu kama Lowasa,Sumaye nimeshiriki kuwatoa CCM na kuwaingiza CHADEMA.Leo nikienda CCM watanielewaje"? Alihoji Mhe Kubenea.

"Absalom Kibanda Ndiye mwanzilishi wa hizi propaganda za mimi kuhamia CCM.Nilimuonya asinichafue kwani namheshimu" amesema Kubenea.

"Mbunge Godbless Lema ndiye amekuwa kinara kuzungumza haya mambo kwenye mitandao ya mimi kuhama hivyo kuleta taharuki kwenye mijadala ya wabunge wa CHADEMA". Amesema Kubenea.

No comments:

Post a Comment

Popular