Kampuni ya Mwananchi waongea na waandishi wa habari juu ya hatua watakazo chukua juu ya mwandishi wao kupotea. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 December 2017

Kampuni ya Mwananchi waongea na waandishi wa habari juu ya hatua watakazo chukua juu ya mwandishi wao kupotea.

 Kampuni ya Mwananchi Communications imesema hadi sasa hawajapata taarifa yoyote kutoka jeshi la Polisi mkoa wa Pwani tokea walipotoa taarifa za kupotea kwa mwandishi wake Azury Gwanda katika kituo chake cha kazi huko Kibiti mkoani wa Pwani wiki mbili zilizopita

Kwa mujibu wa mkewe, Anna Kinoni alichukuliwa na watu ambao hawafahamu eneo ambalo hupenda kukaa na rafiki zake huko Kibiti aa 4 asubuhi Novemba 21

Watu hao walikuwa na gari nyeupe aina ya Toyota Landcruiser walienda eneo alilokuwepo kisha wakaenda nae shambani alipokuwa mkewe, walipofika shambani Azory alimuuliza mkewe ziko wapi funguo za nyumba yao na kuelekezwa

Baadae watu hao waliondoka na Azory na kumuacha shambani mkewe na kusema atarudi jioni ya siku hiyo ya Jumanne Novemba 21 au siku iliyofuata

mkewe alirudi na kukuta nyumba imepekuliwa na vitu vimerushwa shaghalabaghala

siku iliyofuata simu zake zilikuwa hazipatikani

Alhamisi Novemba 23 alienda kuripoti kituo cha polisi Kibiti na polisi kusema hawajui alipon na kumpa RB ila sasa bado hawajatoa taarifa

Mwananchi walipata taarifa za kupotea kwa mwandishi huyo Novemba 30 mwaka huu kutoka kwa ndugu zake na mkewe

MCL walifuatilia hadi kwa kamanda wa polisi mkoawa Pwani na alisema atafuatilia na atatoa taarifa mpaka leo hawajapata taarifa

Juhudi ziliendelea ambapowalitoa taarifa kwa vyombo vya habari vya nje na ndani

Wamaeandika barua kwa waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Spika wa Bunge la Tanzania, Jukwaa la Wahariri TEF, Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari MOAT Nissatan Baraza la Habari Tanzania MCT , Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC na Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC na wadau wengine kuhusu kupotea kwa mwandishi huyo

Pia wameandika barua kwa polisi kuomba kibali cha kuandamana kwenda kwa IGP na wameomba watu wajitokeze kuunga mkono kwenye maandamano hayo

No comments:

Post a Comment

Popular