Jeshi la polisi limeamua kuachana na Dkt Louis Shika yule msomi aliyefikia bei ya kununua majengo matatu ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es salaam Said Lugumi.
Novemba 9,2071 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Saudi Lugumi zilizopo Mbweni JKT na nyingine Upanga jijini Dar es salaam ambazo zote Dkt Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa sh 3.2 bilioni.
Hata hivyo, msomi huyo wa taaluma ya udaktari kutoka nchini Urusi alishindwa kulipa asilimia 25 kwa mujibu wa taratibu za minada na hivyo kukamatwa kisha kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa siku kadhaa kabla ya kuachiwa kwa kujidhamini mwenyewe.
Akizungumza na kulunzifikra blog Jana, kamanda wa polisi Manda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa alisema kesi waliyomfungulia Dkt Shika ya kuharibu mnada hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba za Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo.
Kamanda Mambosasa alisema kesi hiyo haina mashiko kwa kuwa msomi huyo hajatia
hasara yoyote.
Kamanda Mambosasa alisema Dkt Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezi wake ni mdogo na kupeleka kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba.
"Dkt Shika ni mtu wa kumuonea huruma hana kitu, tulisema tunamchunguza na baadae tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko, ndiyo maana hatuendelei na kesi hiyo",alisema kamanda Mambosasa.
Katika mnada huo msomi huyo aliyejizolea umaarufu baada ya tukio hilo alifikia bei ya kununua nyumba za Mbweni JKT kwa sh 900 milioni na nyingine sh 1.1 bilioni na huku ya Upanga alifikia bei ya sh 1.2 bilioni.
.

No comments:
Post a Comment