Aliyekuwa kigogo wa FFU jela kwa kosa la wizi wa SMG nane. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 December 2017

Aliyekuwa kigogo wa FFU jela kwa kosa la wizi wa SMG nane.

Aliyekuwa mkuu wa kikosi cha polisi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Tabora mrakibu msaidizi wa polisi, Bhoke Bruno na wenzake sita Jana jumatano walihukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano jela kwa kosa la kuiba bunfuki nane aina ya SMG, mali ya jeshi la polisi ambaye ni mwajiri wao.

Wengine waliohukumiwa kigungo hicho, katika hukumu iliyosomwa na kaimu msajili wa mahakama kuu kanda ya Tabora Sharwira Sarwatt, watuhumiwa hao ni koplo Idd Abdallah, PC Mwinyi Gonga na Said Mgamela wote kutoka kikosi cha FFU mkoa wa Tabora.

Kwa pamoja watuhumiwa hao waliokuwa waajiriwa wa jeshi la polisi kwa pamoja walitiwa hatiani kwa makosa matatu ambayo ni kula njama, kuiba na kushindwa kuzuia tukio.

Mahakama pia iliwapa adhabu kama hiyo washtakiwa wengine watatu ambao ni Shaban Haruna, Shaban Kabanika na Idd Supu waliodaiwa kushirikiana na waliokuwa maofisa wa jeshi la polisi.

Washtakiwa wengine watatu kati ya kumi waliokuwa wakishtakiwa ambao ni Charles Abihud, Emmanuel Festo na Nicholaus Mlewa waliachiwa huru baada ya ushahidi dhidi yao kukosekana.

"Ushaidi uliowasirishwa na upande wa jamhuri umethibitishia mahakama pasipo shaka kuwa washtakiwa saba kati ya kumi walihukana makosa yanayowakabili, hivyo wanahukumiwa kifungo cha miaka mitano kila kosa", amesema Serwatt.

Kutokana na adhabu ya makosa yote matatu yanaenda pamoja, washtakiwa watakaa magereza kwa miaka mitano.

Awali upande wa mashtaka uliongozwa na wawili mwandamizi wa serikali,Juma Masanja uliiambia mahakama kuwa kwa pamoja washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya April 2013 hadi April 2014.

Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa washtakiwa kwa nyakati tofauti walikula njama ya kuiba bunduki aina ya SMG zilizokuwa zikihifadhiwa katika ghala la kituo cha FFU mjini Tabora.

Upande wa mashtaka ulidai katika shtaka la pili kuwa katika kipindi hicho washtakiwa kwa pamoja bila kuwa na uhalali walichukua bunduki nane kwenye ghala hilo,wakati shtaka la tatu likiwa ni kushindwa kuzuia uhalifu kutendeka.

No comments:

Post a Comment

Popular