Wabunge wameiomba serikali iliangalie kwa jicho la pekee tatizo la uhaba wa watumishi wa afya, hususani wauguzi na madaktari bingwa katika vituo, zahanati na hospitali na kulipatia ufumbuzi.
Pamoja na hayo, wabunge pia wamebainisha juu ya umuhimu wa serikali kuongeza jitihada za kutekeleza mpango wake wa kujenga zahanati katika kila kata kwa kuwa bado yapo maeneo ambayo hayana zahanati na kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Wabunge waliyasema hayo bungeni mjini Dodoma Jana wakati wakichangia mjadala wa kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka 2018/19.
Mbunge wa Mikumi,Mhe Joseph Haule (Chadema) alisema wilayani Kilosa hali ya upungufu wa watumishi ni kubwa kwani hadi sasa kuna mahitaji ya watumishi 1,025 na waliopo ni 474 tu sawa na asilimia 46.
Mhe Haule alisema tatizo hilo limeongezewa uzito zaidi na utaratibu wa kupunguza watumishi wenye vyeti feki na hivyo kusababisha uhaba wa madaktari na wauguzi katika vituo vya afya, zahanati na hospitali ya Kilosa.
Naye Mbunge wa Kuteuliwa, Mhe Salma Kikwete (CCM) alisema afya ndio msingi wa maendeleo katika nchi yoyote endapo kuna ukosefu wa afya, uchumi wa eneo husika utapungua kwa kukosa nguvu kazi.
Hata hivyo, alisema Mkoa wa Lindi mpaka sasa haujafahamu hatma yake ya kuwa na hospitali ya mkoa na wilaya, kwani hospitali iliyopo ya Sokoine imekuwa ikiitwa ya mkoa na wilaya na hivyo kuleta mkanganyiko.
“Pamoja na mkanganyiko huu bado mkoa huu una tatizo kubwa la uhaba wa wataalamu wa afya. Ni asilimia 28 pekee ya wataalamu wa afya ndio wapo Lindi na hivyo kuwa na upungufu wa asilimia 72 ya wataalamu hao,” alisisitiza Mhe Salma Kikwete.
Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe Amina Makilagi (CCM), alisisitiza juu ya umuhimu wa serikali kuliangalia tatizo la uhaba wa wataalamu wa afya kwa kuwa hospitali nyingi nchini zinakabiliwa na hali mbaya ya uhaba wa watumishi hao.
Kwa upande wake, Mhe Mariam Kisangi (Viti Maalumu - CCM), aliiomba serikali kuboresha hali ya matibabu katika Hospitali ya Mloganzila nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuiongozea wataalamu zaidi wakiwemo madaktari bingwa na wauguzi kwa kuwa kwa sasa hospitali hiyo inazidiwa na wagonjwa.
Mbunge wa Vunjo (NCCRMageuzi), Mhe James Mbatia alisema ni wakati sasa wa serikali kuanza kushirikisha sekta binafsi na wawekezaji wakubwa wa ndani na nje ya nchi ili wawekeze katika sekta ya afya na kuongeza ubora wa huduma za afya nchini.
“Tuwe wakweli japo wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa, hatujawawezesha kibajeti ili waweze kufanya kazi yao. Serikali inabidi iweke mazingira rafiki na motisha kwa sekta binafsi wavutiwe ili wawekeze kwenye sekta hii", alisema Mhe Mbatia.

No comments:
Post a Comment