Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Mhe Freeman Mbowe ametua bungeni mjini Dodoma leo kuongoza kikao ambacho pamoja na mambo mengine kimetoa msimamo wa wabunge wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), kushiriki au kutoshiriki vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.
Mhe Mbowe pamoja Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ambao pia ni miongoni mwa viongozi wa chama hicho waliopata dhamana Jana katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi saba wa chama hicho, wamewasili bungeni leo mchama na kuingia moja kwa moja katika Ukumbi wa Msekwa kwa ajili ya kikao hicho.
Baadhi ya wabunge wamesema kikao hicho kinatarajia kutoa hatma ya kambi hiyo kushiriki mkutano huu wa Bunge la Bajeti na masuala mengine ambayo yatatikisa.
Tangu kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti juzi Jumanne, wabunge wa upinzani wameonekana kususia bunge hilo huku idadi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) pelee wakionekana kwa uchache wakati viti vya wabunge wa Chadema vikiwa vitupu.
PianKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), imesema haitasoma hotuba wala taarifa zake bungeni endapo utaratibu wa kuziwasilisha kwa Katibu wa Bunge hatua ya kuhaririwa kwanza kabla ya kusomwa bungeni itaendelea.
Pamoja na hayo, wamesema hawatatusa bunge kwa ajili hiyo wala sababu nyingine yoyote.
Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe Freeman Mbowe amesema hayo Leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge na kuhusu kukataliwa kusomwa kwa hotuba yao bungeni leo.
Mhe Mbowe amesema anamshangaa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kukataa kutosomwa kwa taarifa ya kambi hiyo bungeni leo kwa sababu tu haikuwasilishwa kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni.
“Naibu Spika anasema hotuba ya KUB haipo wakati anajua kambi ilikuwa ina watumishi wanne ambao walikuwa wanafanya utafiti, kuandaa randama ya serikali, kuandaa hotuba zote zikiwamo za serikali sasa watumishi hao tangu Desemba mikataba yao iliisha na niliandika dokezo kuomba wapewe mkataba upya hadi sasa Katibu wa Bunge amekataa kufanya hivyo akidai Spika wa Bunge yuko nje kwa matibabu", amesema Mhe Mbowe.
“Sawa walitaka hotuba hiyo niiandikie Segerea, kwa sababu wale vijana ndiyo walikuwa wakifanya hayo na bunge lina watumishi wa mikataba 30 wakiwamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wote wana mikataba ya miaka miwili miwili lakini wengie wako ofisini isipokuwa wa kambi ya upinzani ambao walikufukuzwa kama mbwa katika bunge la Januari,” amesema Mhe Mbowe.
Pamoja na mambo mengine, Mhe Mbowe amesema hapatakuwa n ahotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni hadi watumishi wa warejeshwe lakini pia hata watakaporejeshwa, hawatakuwa tayari kupeleka hotuba zao kwa katibu wa Bunge akachague ni nini cha kusoma bungeni na nini cha kuacha na kwamba Bunge liking’ang’ania kufanya hivyo, hawatasoma hotuba hizo.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai alisema bunge lina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge na ofisi zao.
Alisema hadhani kama aliyozungumza Mhe Mbowe yatakuwa na ukweli wowote kwa sababu bunge linahudumiwa na Sekretarieti ya Bunge na watumishi wake walioajiriwa na kuhudumia wabunge.
“Hatujakosa sekretarieti, nina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge.
Kulikuwa na watumishi wa mkataba ambao mkataba wao ulimalizika Desemba, sasa alitakiwa kusema kama anawahitaji hao lakini mwenye uwezo wa kusema waendelee au wasiendelee ni Tume ya Utumishi wa Bunge.
“Kwangu alikuja akaniambia lakini sasa mimi ni mtumishi wa Bunge na kama unavyofahamu Spika wa Bunge alikuwa nje kwa matibabu", amesema Kagaiga
“Watumishi walioajiriwa na Bunge wapo, mimi nikiwa mmojawapo kama mbunge anawahitaji anapewa lakini si kwa kazi binafsi. Kama anataka watumishi wa bunge kumhudumia yeye peke yake hiyo ni juu yake, wanaweza kuwa hawataki lakini sisi hatuwezi kuwalazimisha,” amesema Kagaigai.
Vile vile Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mhe Freeman Mbowe amesema amenyang’anywa gari la serikali alilokuwa akitumia na Ofisi ya Bunge ambalo ni haki yake kuwa nalo.
Pia Mhe Mbowe amesema amenyang’anywa gari hilo tangu Januari, mwaka huu.
“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu", amesema Mhe Mbowe.
“Lakini mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” amesema Mbowe bila kuelezea zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo", amesema Mhe Mbowe.
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.
“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” amesema Kagaigai.

No comments:
Post a Comment