Spika Ndugai ataja sifa za Mbunge kutibiwa nje ya Nchi. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 19 April 2018

Spika Ndugai ataja sifa za Mbunge kutibiwa nje ya Nchi.

 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai amesema ili Mbunge aweze kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za Bunge anapaswa kuwa na vibali vitatu; kibali cha Bunge, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Rais Magufuli.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Mhe Godbless Lema aliyehoji sababu za Bunge kushindwa kutoa gharama za matibabu za mbunge wa chama hicho Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu.

"Kuna siku nitataja orodha ya wabunge wanaotibiwa nje ya nchi. Ni lazima wawe na vibali hivi. Rais alishasema wazi kuwa anazuia safari za nje zisizokuwa na lazima", amesema Spika Ndugai.

"Mhe Lissu alipelekwa Nairobi katika matibabu kwa utaratibu ambao haukuwa na kibali cha Bunge. Hili jambo nimeshalisema sana sijui kwanini linajirudia, "amesema na kuongeza Spika Ndugai.

“Nashukuru Mhe  Lissu anaendelea na matibabu na ninajua kuna Wajerumani wanamsaidia" amesema Spika Ndugai.

No comments:

Post a Comment

Popular