Rais Magufuli atoa wito kwa Watanzania. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 1 April 2018

Rais Magufuli atoa wito kwa Watanzania.


Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakiishi kwa kushirikiana ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.

Rais Magufuli amesema hayo Leo Aprili mosi baada ya kuungana na wakristo wote nchini katika maadhimisho ya misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika kabisa la Mtakatifu Joseph Jimbo kuu la Dar es salaam.

Rais Magufuli amesema: "kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu kristo ukafufue matendo yetu, tukaendelee kuijenga amani yetu, upendo wetu na tujenge maendeleo ya Watanzania wote, kwani Yesu kristo ametufundisha miongoni mwetu".

"Kwahiyo nashukuru sana kwa baba padri kwa kutuongozea misa hii naomba shukrani zangu uzifikishe kwa Kardinali Pengo, maaskofu wote na Watanzania tuendelee kusimamia kwa pamoja amani yetu ili tulijenge Taifa letu", amesema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Popular