Usiku wa Aprili 9, 2018, hautasahaulika kwenye historia ya Ndabacha Simon (23), mama wa watoto watatu aliyefukiwa na kifusi cha nyumba yao kwa saa nne.
“Halikuwa jambo rahisi, nilihisi jasho linanitoka mwili mzima, sauti ilikatika, nguvu ziliniishia nikahisi na mimi nakufa na watoto wangu,” anasema Ndabacha.
Mkazi huyo wa mtaa wa Buguku Mkolani jijini Mwanza, ambaye amepoteza watoto wake wawili katika tukio hilo anasimulia namna alivyonusurika baada ya kufukiwa na kifusi kwa saa nne.
Ndabacha anasema hayo yote yamesababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa Aprili 9 na kwamba, hataweza kuisahau kwenye historia ya maisha yake baada ya kuwapoteza watoto wake wawili kwa wakati mmoja.
Anasema siku ya tukio nyumbani kwake kulikuwa na watu watano akiwamo mama yake mzazi, Tabu Lukuba (65), mtoto wake wa kiume, Samson Simon (5) na hao waliokufa ambao ni Mariam Simon (4) na Mussa Baraka (2).
“Mvua ilianza kunyesha saa nane usiku ilipofika saa tisa nilisikia udogo unaanguka, ghafla ukuta mzima ukatuangukia na kutufunika, hatukuwa na namna ya kujiokoa, mimi na wanangu tukaanza kupiga kelele za kuomba msaada lakini kutokana na mvua hatukuweza kusaidiwa,” anasema Ndabacha na kuongeza:
“Kutokana na juhudi za kuomba msaada kugonga mwamba, niliona watoto wangu mmoja baada ya mwingine wakikata roho; mdogo ambaye ni Mussa nilisikia sauti moja tu akisema mama nisaidie nakufa, kweli akakata roho.”
Anasema ilipofika saa kumi alfajiri mtoto mwingine, Mariam naye alisikia akikoroma mara moja akajua kuwa naye tayari amekufa.
Juhudi za kuokolewa
“Haikuwa jambo rahisi, nilisubiri kwa muda wa saa nyingine mbili hadi jirani yangu alipofungua mlango wa geti lake, nikaanza kumuita nikimuomba aniokoe.
“Baada ya kufika naye ilimlazimu awapigie simu majirani wengine ambao walianza juhudi za kutuokoa na kufanikiwa kututoa watatu,” anasema.
Anasema waliookolewa walikuwa watu wazima watatu; yeye (Ndabacha) mama yake mzazi na mtoto wake mkubwa wa kiume.
“Baadaye mwenyekiti wa mtaa na wananchi walitupeleka katika Hospitali ya Wilaya Nyamagana kwa ajili ya matibabu, tuliruhusiwa baada ya afya zetu kuimarika,” anasema Ndabacha.
Maisha anayoishi
Ndabacha ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya Simon, yeye na kaka yake hawakuendelea na masomo ya sekondari kutokana na hali duni ya maisha.
Anasema baada ya baba yake mzazi kufariki dunia, walilazimika kuuza shamba ili kujikimu kimaisha hivyo wakalazimika kuishi katika nyumba za kupanga.
“Baba yangu aliugua ugonjwa ambao haukujulikana hospitalini, baadaye tukamtoa na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji ambaye alimtibu na kutuomba tumpatie Sh300,000,” anasema Ndabacha.
Hata hivyo, Ndabacha anasema hali ya ugonjwa wa baba yake ilijirudia na alipoteza maisha.
“Tangu siku hiyo mimi na kaka yangu tumekuwa watu wa kujishughulisha na kazi ndogondogo, mfano mimi nauza karanga, kaka anatafuta vibarua au anakodi pikipiki anaendesha akipata fedha wanagawana na mmiliki,” anasema.
Anasema fedha inayopatikana inawasaidia kupanga nyumba ambayo wanalipia Sh30,000 kwa miezi sita.
Anaiomba Serikali iangalie namna ya kuwasaidia sehemu ya kuishi kwa sasa, kwa kuwa hawana fedha ya kuendelea kupanga.
Uongozi wa mtaa
Mwenyekiti wa mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa, Maduhu Sultani anasema alipata taarifa hizo saa moja asubuhi kutoka kwa balozi wa mtaa huo, baada ya kufika eneo la tukio alihakikisha anawasaidia kuwapeleka hospitali kwa ajili ya matibabu.
Sultani anasema kwamba katika mtaa huo hakuna madhara mengine yaliyotokea tangu mvua hiyo ianze zaidi ya hayo na kwamba, ni tukio la aina yake ambalo halitasahaulika vichwani na machoni mwao.
Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi anasema kwamba tukio hilo limesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, huku akiwataka wanaoishi maeneo ya mabondeni kuhama kwa kuwa mvua hizo bado zinaendelea.

No comments:
Post a Comment