Wabunge wametaja baadhi ya kero za Muungano wakitaka zitafutiwe ufumbuzi.
Miongoni mwa kero zilizitajwa na jana bungeni mjini hapa katika mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) mwaka 2018/19 ni bidhaa kutoka Zanzibar kuzuiwa kuingia katika soko la Bara, vikwazo katika biashara ya pamoja na hadhi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano katika sherehe za Mapinduzi.
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Mhe Zitto Kabwe alisema, “Kuna kasoro katika suala la bidhaa za Zanzibar kuingia katika soko la Tanzania Bara,”
“Iweje leo tuanze kuzungumza kuondoa vikwazo vya biashara wakati katika hali ya kawaida ilitakiwa bidhaa zote zinazozalishwa Zanzibar ziingie moja kwa moja katika soko la Tanzania Bara bila vikwazo vyovyoto", alisema Mhe Zitto kabwe.
“Leo Serikali inasema inazuia sukari kutoka Zanzibar kwa sababu ya kuzuia magendo, lakini Tanzania Bara inayozalisha sukari mkoani Kagera na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi, inaruhusu Kagera kuuza sukari Uganda. Iweje Zanzibar izuiwe kuingia sukari huku (Bara)?”alihoji Mhe Zitto kabwe.
Pia Mhe Zitto kabwe alisema kama kuna kasoro yoyote iliyobainika, wataalumu na maofisa wa biashara walipaswa kwenda Zanzibar kuangalia kinachozalishwa ili watoe uamuzi wa bidhaa hizo kuingia Tanzania Bara.
Mbunge wa Magomeni (CCM), Mhe Jamal Kassim Ali alizungumzia mikopo ya nje na kubainisha kuwa suala hilo linasimamiwa na Serikali ya Muungano lakini kumekuwa na ucheleweshwaji wa kutoa kibali cha mikopo kwa miradi ya kimkakati ya Zanzibar.
Mhe Jamal alisema umeombwa mkopo kwa ajili ya kuendeleza jengo la Terminal II katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar pamoja na Bandari ya Mpigaduri, lakini mpaka sasa kibali cha kuomba hakijatolewa.
Pia Mhe Jamal alisema moja ya sababu za Muungano ni fursa ya biashara kutoka pande zote mbili, jambo ambalo kwa sasa lina changamoto ambazo hazikuwepo miaka ya 90 ambako Zanzibar ilikuwa ikiuza zaidi bidhaa zake Bara.
“…Leo vitu vikija bara ndio kunakuwa na TBS (Shirika la Viwango Tanzania) na TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa) ila vitu vya Bara vinakuja Zanzibar bila tatizo lolote. Hizi changamoto zimechukua muda mrefu kutatuliwa,” alisema huku pia akigusia changamoto ya kodi ya forodha, kwamba mtu akinunua bidhaa Tanzania Bara kwenda Zanzibar anatozwa kodi.
Mbunge wa Temeke (CUF), Mhe Maulid Mtolea alihoji kuhusu hadhi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano anapohudhuria sherehe za kitaifa visiwani Zanzibar akisema anapokwenda kuhudhuria sherehe za Mapinduzi hapigiwi mizinga 21 huku na badala yake anayepigiwa ni Rais wa Zanzibar.
“Nawapaongeza Wazanzibari kwa namna ya umoja wao wa kuipigania Zanzibar yao bila kuzingatia wanatokea upande upi wa kisiasa, ndio maana wenzetu wanafanikiwa. Watu wanahisi Tanzania Bara hakuna kero za Muungano lakini ukweli ni kwamba kero za upande huo hazina pa kwenda, hakuna pa kuzisemea", alisema Mhe Mtolea.
Mhe Mtolea alisema ili Muungano uwe imara, ni lazima kupunguza manung’uniko kutoka pande zote mbili.
“Kuwafurahisha Watanzania Bara si kuwabana Wazanzibari, ni kuwaacha Watanzania Bara nao waseme,” alisema Mhe Mtolea.
“Kwa nini tunayapora mamlaka ya Rais kuhudhuria sherehe za Mapinduzi. Katiba ibara ya 33 (1),(2) inamtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa ndiye kiongozi mkuu wa nchi lakini anapokwenda kwenye sherehe za Mapinduzi anaingia wa pili na wa Zanzibar anaingia mwishoni.” alisema Mhe Mtolea jambo hilo halipo sawa kiitifaki.
Majibu ya waziri
Akijibu hoja za wabunge, Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe Januari Makamba alisema Serikali haina uwezo wa kuzuia Zanzibar kupata mikopo wala kutoheshimu Muungano.
Mhe Makamba alisema historia ya Muungano ni biashara, huku akitolea mfano jinsi watu wa pande hizo mbili wanavyofanya biashara. Kuhusu ushuru wa forodha alisema wametengeneza mfumo wa pamoja wa uthamini wa kodi ambao bado haujatumika na kwamba chini ya mfumo huo viwango vya kodi vitakuwa sawa pande zote.
Kuhusu biashara za Zanzibar kutoruhusiwa kuingizwa Tanzania Bara alisema tayari vikao vimeshakaa kujadili suala hilo na kuna baadhi ya mambo wameshayatatua na mengine yapo katika hatua za utatuzi.
Kuhusu mkopo wa kiwanja cha ndege Zanzibar, alisema Kamati ya Madeni ya Taifa itakaa kupitia mkopo wa Dola 58 milioni za Marekani kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Terminal II visiwani humo.
Hata hivyo, bila kuzitaja, Makamba alisema hoja nyingine zilimshangaza na kusema zipo atakazozijibu kwa maandishi.
Awali, Mhe Makamba alisema chini ya uongozi wa Rais John Magufuli na Dk Shein, Muungano unaendelea kuimarika na kushamiri.
“Chini ya uongozi wao, hakuna changamoto yoyote inayoweza kutufarakanisha, kututenganisha wala kuturudisha nyuma… kwa watu wa itikadi zote na kutoka pande zote za Muungano, mjadala sio uhalali wa Muungano, bali mbinu za uuimarisha,” alisema Mhe Makamba.

No comments:
Post a Comment