Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekosoa utaratibu wa Serikali kuhamisha baadhi ya walimu wa shule za sekondari kufundisha shule za msingi kwa maelezo kuwa kila ngazi ya ualimu ina miongozo na mafunzo yake mahsusi.
Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2018/19 kwa niaba ya mwenyekiti, Peter Serukamba, mbunge wa Nzega Mjini, Mhe Hussein Bashe amesema Serikali inatakiwa kuliangalia suala hilo kwa jicho la pekee.
“Kamati inatambua na kuelewa tatizo la ukosefu wa walimu hasa katika shule za msingi hapa nchini, ila kuchukua walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi si sawa,” amesema Mhe Bashe.
Mbunge huyo ameyasema hayo Jana Aprili 30, 2018 bungeni Jijini Dodoma.
“Kumchukua mwalimu wa sekondari kwenda kufundisha shule ya msingi kumepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa jamii na walimu wenyewe ikiwemo kuhisi kuadhibiwa hivyo kushusha morali ya kufanya kazi.”aamesema Mhe Bashe.
Aidha Mhe Bashe amesema Serikali inapaswa kutazama uamuzi huo kwa jicho la pekee na kufanya uamuzi ulio sahihi kwa mustakabali mzuri wa elimu nchini.
Pia Mhe Bashe amesema kamati hiyo ina taarifa kuwa mahitaji ya walimu kwa shule za msingi ni 273,454 lakini walimu waliopo ni 175,946 na hivyo kuwa na upungufu wa walimu 97,508 sawa na asilimia 35.
“Kwa shule za sekondari hasa masomo ya sayansi, mahitaji ni walimu 35,136 lakini waliopo ni 19,285 na hivyo kuwa na upungufu wa walimu 15,851 sawa na asilimia 45.1,” amesema Mhe Bashe.

No comments:
Post a Comment