Hoja ya mbunge wa Jimbo la Kawe (Chadema), Mhe Halima Mdee kuhusu Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Jana iliibua mvutano bungeni kati yake, wabunge na mawaziri.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19, Mhe Mdee alisema amesoma taarifa za Msajili wa Hazina na ATCL zinazoonyesha shirika hilo lina madeni, haliwezi kujiendesha kibiashara na halijafanyiwa hesabu kwa muda mrefu.
Kilichoibua mvutano hadi kurushiana vijembe ni hatua ya Mdee kumtaja Rais John Magufuli akisema ikigundulika fedha zilizowekezwa katika ununuzi wa ndege hazijafuata utaratibu hata kinga aliyonayo ya kutoshtakiwa inaweza kuwa shakani.
Kauli ya mbunge huyo iliwainua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe Stella Manyanya waliomtaka kuheshimu jina la Rais na kwamba halipaswi kutumiwa kwa dhihaka.
Mchango wa Mhe Mdee
Akichangia Mhe Mdee alisema, “Nikiangalia kitabu hapa naona Serikali inataka kufanya ununuzi wa ndege mpya kwa ajili ya ATCL. Tukumbuke mwaka jana (2017/18), Serikali kupitia Waziri wa Fedha ilitenga bilioni zisizopungua 500 kwa ajili ya kununua ndege,” alisema Mhe Mdee.
“Hoja si kupinga ununuzi wa ndege, hoja hapa ni fedha tunazowekeza ambazo ni kama Sh1 trilioni. Je, zinakwenda kuzalisha au tunakwenda kuzitupa na kupotea", alisema Mhe Mdee.
Huku akisoma taarifa za Msajili wa Hazina na ile ya ATCL, Mhe Mdee alisema, “Hii ya Msajili Hazina anasema ameshindwa kufanya uchambuzi wa kina wa utendaji kazi wa ATCL kutokana na kutokuwepo kwa taarifa za kutosha. Kwa mfano, hesabu za shirika zilizokamilika ni za mwaka 2014/15 zilizofanywa na PWC. Hata hivyo, hesabu hizo hazikuwa zimepitiwa na bodi.”
Mhe Mdee alisema hali hiyo imesababisha ofisi ya msajili huyo kushindwa kuchambua na kubainisha hali halisi ya uwekezaji ilivyo hadi sasa.
“Kuhusu madeni ya shirika (msajili) anasema ameshindwa kujua hali ya ukwasi kwa sababu ya shirika kutokuwa na hesabu za muda mrefu. Taarifa ya ATCL inasema shirika halikuwa na mpango wa biashara, sasa tunawekezaje fedha hapa,” alihoji Mhe Mdee.
Mhe Mdee alisema Januari wataalamu wa Serikali wanaosimamia mashirika walisema ATCL ina madeni ya Sh317 bilioni. Alisema Serikali ni vyema ingewekeza katika kilimo, sekta ambayo inahusisha asilimia 75 ya Watanzania.
“Msije mkajiona mko salama. Tukigundua mmeziwekeza kinyume na utaratibu kama nyaraka zinavyoonyesha tutawachukulia hatua. Ni muhimu Rais akajua hiyo…, kama kuna mambo aliyofanya makusudi kwa kuona hakuna usalama mbele tutamshughulikia. Naongea kwa dhamira ya dhati najua wabunge wengi wanajua,” alisema Mhe Mdee.
Mawaziri wampinga
Baada ya kauli hiyo, Naibu Waziri Mhe Manyanya alisimama na kutoa taarifa kwa Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai akimpinga Mhe Mdee na kumtaka kuliheshimu jina la Rais kwa kuwa ni kiongozi anayeheshimiwa na watu wote.
“Upinzani wamekuwa wa kulalamika badala ya kutoa mawazo mbadala. Mbona wabunge wa upinzani kipindi cha nyuma walikuwa wakichangia kuhusu ATCL na ndege zetu, wengine mmekuwa kama hamkumbuki?” alihoji Mhe Manyanya.
Akiunga mkono maelezo ya Mhe Manyanya, Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Lukuvi alinukuu kanuni ya 64 ya Bunge na kubainisha kuwa jina la Rais halipaswi kutumika kwa dhihaka katika mjadala kwa madhumuni ya kutaka kulishawishi Bunge kuamua jambo lolote.
“Jina la Rais halipaswi kutumika namna hiyo, neno kumshughulikia Rais kwa maoni yangu halihusiani na mjadala huu. Mbunge aondoe maneno yake na kujielekeza katika mjadala,” alisema Mhe Lukuvi.
Akijibu hoja hiyo, Mhe Mdee alisema, “Rais alichaguliwa na Watanzania, hili Bunge ni la wawakilishi wa Watanzania. Rais lazima akosolewe na jina lake lazima litajwe kama anakwenda kinyume na utaratibu. Ile dhana kuwa Rais haguswi lazima iishe. Bunge likiogopa kumtaja Rais wakati sisi tunapitisha bajeti na Rais ni sehemu ya Bunge, tunalifanyia makosa Taifa hili. Sijatumia jina la Rais kwa kebehi.”
Wabunge wamshukia
Wakati Mhe Mdee akiendelea kuzungumza, mbunge wa Siha (CCM), Dkt Godwin Mollel alitoa taarifa na kumkosoa akisema mapato ya asilimia 100 ya Chadema hayaonekani na kwamba inaendeshwa kwa michango ya wabunge na ruzuku huku akibainisha kuwa haiwezi kuongoza Serikali.
“Chadema hawana hata kibanda kwa ajili ya kupata kipato. Hata kama mnaweza kuwa na mawazo mazuri kwa miaka yote mmefanya nini ili tuamini mkichukua Serikali tuone mnaweza kufanya kitu?” alihoji Dkt Mollel na kujibiwa na Mdee, “Siwezi kumjibu Dkt Shika bidhaa ya Kichina nitakuwa najidhalilisha.”
Wakati Dkt Mollel akizungumza,Mhe Mdee alikuwa akitaka kumkatisha jambo ambalo lilimnyanyua Spika Ndugai na kumtaka mbunge huyo wa Siha kueleza kwa kina kauli yake kwa kuwa hajamsikia vizuri.
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Mhe Joseph Msukuma alitoa taarifa akimpinga Mhe Mdee kutumia Jina la Dkt Shika kwa kuwa linamdhihaki Dkt Mollel.
Wakati Mhe Mdee akijiandaa kujibu taarifa hiyo, alisema ametukanwa na mbunge wa Mtera (CCM), Mhe Livingstone Lusinde. “Mhe Spika nimetukanwa. mhe Lusinde amenitukana tusi zito sana sasa kama hajafuta na mimi nitatoa la kwangu,” alisema Mhe Mdee. Hata hivyo, hakueleza tusi alilotukanwa.
Wakati Mhe Lusinde akisimama na kuwasha kipaza sauti na kutamka kufuta ‘tusi’ hilo, Ndugai aliwataka wabunge kumuacha Mhe Mdee azungumze. Hata hivyo, alipoanza kuzungumza Ndugai alimkatisha na kumueleza kuwa muda wake wa dakika 10 wa kuchangia umekwisha.
Ndugai awakingia kifua mawaziri
Katika hatua nyingine, Spika Ndugai aliwakingia kifua mawaziri wanaojibu hoja kuhusu wizara zao zilizoibuliwa katika ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka 2016/17, akisema haoni tatizo lolote na kuwataka kuendelea kufanya hivyo.
Alitoa kauli hiyo akijibu mwongozo wa mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara aliyehoji uhalali wa mawaziri hao kumjibu CAG.
Tangu CAG alipowasilisha taarifa hiyo mwezi huu bungeni, mawaziri kadhaa wameshamjibu jambo ambalo limeibua mjadala huku mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Nagwenjwa Kaboyoka akisema walipaswa kutoa majibu hayo kwenye kamati.

No comments:
Post a Comment