Esther Bulaya ashikiliwa na Jeshi la polisi. - KULUNZI FIKRA

Friday, 13 April 2018

Esther Bulaya ashikiliwa na Jeshi la polisi.

 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe  Freeman Mbowe na Katibu wake, Dkt Vincent Mashinji wameondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi central baada ya kuripoti, huku Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini,Mhe  Esther Bulaya ikidaiwa atalala mahabusu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Wengine waliondoka kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa Habari,Dkt  Mashinji amesema kuwa wameripoti kituoni hapo kama walivyoamriwa na mahakama, lakini wameambiwa Mbunge wa Bunda mjini Mhe Esther Bulaya atabaki mahabusu kwa ajili ya upelelezi.

“Mhe Esther Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu,” amesema Dkt Mashinji.

No comments:

Post a Comment

Popular