CAG ametoa taadhari kwa Serikali. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 11 April 2018

CAG ametoa taadhari kwa Serikali.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema, ingawa kiwango cha ukopaji kinapungua ni lazima kuwa waangalifu kwenye kukopa.

Profesa Assad ameyasema hayo Leo  wakati anazungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma baada ya Serikali kuwasilisha bungeni ripoti sita za ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2017.

Kwa mujibu wa Profesa Assad, ripoti hizo ni Ripoti ya Serikali Kuu, Ripoti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ripoti ya Mashirika ya Umma, Ripoti ya Miradi ya Maendeleo, Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ripoti 10 zinazohusu ukaguzi wa ufanisi katika sekta mbalimbali.

Aidha Profesa Assad amesema, kuna namna tatu ya kupima kiwango cha deni la taifa ikiwa ni pamoja na kuangalia uwiano wa kiwango cha deni na Pato Ghafi la Taifa (GDP).

Profesa Assad amesema, deni pia linaweza kupimwa kwa kuangalia kiwango cha mauzo nje ya nchi, na kiwango cha makusanyo ya kodi.

Pia Profesa  Assad amesema, hadi Juni 30, 2017 deni la taifa lilikuwa shilingi treilioni 46.08 likiwemo deni la ndani la shilingi trilioni 13.33 na ndeni la nje shilingi trilioni 32.75.

Profesa Assad amesema, shilingi trilioni 4.58 hakikujumuishwa katika deni la taifa kwa kuwa madeni ya mifuko ya pensheni hayakujumuishwa sanjari na dhamana ambazo masharti yake yalikiukwa.

No comments:

Post a Comment

Popular