Watu kadhaa wamefariki dunia baada ya basi la abiria la kampuni ya city Boys lililokuwa linatoka Karangwe mkoani Kagera kwenda Jijini Dar es salaam, kugongana uso kwa uso na Fuso iliyokuwa imebeba mzigo wa viazi katika eneo la Igunga mkoani Tabora , tukio ilo limetokea usiku wa kuamkia Leo.
Akizungumza na kulunzifikra blog, kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Tabora , Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutoka kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu waliofariki katika ajali hiyo ni watu 12.
Pia kamanda Mutafungwa amesema Gari T486 ARB FUSO ikiwa na mzigo wa viazi ikitokea Singida kuelekea Igunga mkoani Tabora, tairi ya kulia litumbukia katika mashimo mawili barabarani kisha kupasua tairi na rim kupinda & mfumo wa usukani kukatika maungio ya steering rod na steering box kisha gari kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya City boy.
Vile vile kamanda Mutafungwa amesema Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha , 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya Igunga. Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya Wilaya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi ambapo wanaume wawili wamepelekwa Bugando Mwanza na mwanamke mmoja amepelekwa pia.
Dereva wa basi amefariki papo hapo. Wahusika wa FUSO kwa taarifa za awali inasemekana wamekimbia baada ya ajali hii.

No comments:
Post a Comment