Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema idara yake ya sheria imejiweka ‘mguu sawa’ kuhakikisha viongozi wake wanapata msaada kitaaluma watakapofikishwa mahakamani kwa makosa ya tuhuma wanazohojiwa sasa na Jeshi la Polisi.
Kesho, viongozi saba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe Freeman Mbowe, wataripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, ikiwa ni wiki ya sita tangu waanze kufanya hivyo.
Mbali na Mhe Mbowe, viongozi wengine wa Chadema ambao wametakiwa kuripoti kituoni hapo kwa mara nyingine ni Katibu Mkuu, Dkt Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe John Manyika na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ndugu Salum Mwalimu.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti (Mara, Simiyu na Shinyanga), Mhe John Heche, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha) Taifa, Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti Bawacha Mkoa wa Mara na Mwekahazina wa baraza hilo Taifa, Mhe Esther Matiko.
Akizungumza na kulunzifikra blog Jana Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Mashinji alisema kilio chao cha kila siku ni kupelekwa mahakamani ili haki ikapatikane huko.
“Viongozi wameshahojiwa na wamechukuliwa maelezo, kila mmoja amehojiwa kwa kosa lake... wengine kwa uchochezi, wengine kwa mkusanyiko, sasa wanachoogopa kutupeleka mahakamani ni nini?" Alihoji Dkt Mashinji."Sisi tunataka tupelekwe mahakamani.”
Alisema Chadema ina wanasheria wengi licha ya Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu kuwa katika matibabu nje ya nchi.
Alisema chama kina Mkurugenzi wa Sheria, maofisa wakuu wa Idara ya Sheria na kwamba pia kina wanasheria ambao wataendelea na majukumu ya kuwatetea viongozi wa chama.
Alisema wapo tayari kupelekwa mahakamani licha ya kutofahamu kama watashinda au watashindwa, lakini wanaamini mahakamani ndipo sehemu sahihi haki inapopatikana.
“Sisi imekuwa ni rai yetu siku zote watupeleke mahakamani, kama maelezo waliyachukua, kama hatuna kesi waseme, sisi viongozi hatuwezi kukimbia, lakini siyo kila siku watuambie twende polisi,” alisema Dkt Mashinji.
Dkt Mashinji alisema mahakamani ndiyo chombo kinachoamua kama mshitakiwa ni mhalifu au la, hivyo kitendo cha polisi kuwakamata, kutowapeleka mahakamani na kuwaachia na kuwahitaji waripoti kila wakati ni unyanyasaji.
Kauli ya katibu mkuu huyo inakuja siku tatu tangu Mhe Mbowe adai nchi ina Jeshi la Polisi lakini si huduma za jeshi hilo.
Kauli ya Mhe Mbowe ilikuja kama majibu ya majibu ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa waraka wa mwenyekiti huyo wa Chadema alimodai pamoja na mambo mengine, Polisi ina mpango wa kuwapa kesi ya uhaini viongozi na wabunge wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Katika waraka huo, Mbowe (56), alidai chama chake kimepata taarifa za kiitelijensia kuhusu kupangwa kwa njama mahususi za kuwabambikia viongozi wa chama hicho kesi za mauaji au uhaini kwa lengo la kupunguza nguvu ya upinzani nchini.
KUMKOMOA MTU Hata hivyo, IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi halifanyi kazi kwa ajili ya kukomoa mtu na akasisitiza kuwa Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa wanayohojiwa na jeshi hilo sasa.
Lakini Mbowe alimjibu nchi inapaswa kuwa na Jeshi la Polisi linalotoa huduma kwa raia tofauti na la sasa ambalo alidai halitekelezi jukumu hilo.
"Kama tuna makosa, na sasa ni wiki tano wanatuita kutuhoji na kosa halijajulikana. Wiki ya sita tunakwenda polisi, kila wiki tunakwenda polisi. Hawafungui kesi, hatujui kipi kinaendelea," Mbowe alisema na kueleza zaidi:
"Tatizo la nchi yetu ni kwamba tuna Jeshi la Polisi lakini hatuna huduma ya polisi. Na tumelalamika kuhusu hili na kwenye mabadiliko ya katiba ya nchi tulipendekeza kwamba Jeshi la Polisi lazima litoe huduma kwa raia kwa kutambua kwamba lina wajibu huo.
"Tunapaswa kuwa na Jeshi la Polisi linalotoa 'services' (huduma) badala ya kuwa na Police Force (Jeshi la Polisi).
"Kulifanya Jeshi la Polisi kuwa Police Force maana yake sasa kila mahali ni kutumia nguvu tu badala ya kutumia busara na kuelewa kwamba kila mtu ana haki zake."
Mhe Mbowe alisema Bunge linaendelea na shughuli zake kupitia kamati zake za kudumu lakini yeye na baadhi ya wabunge wa chama chake kwa wiki tano mfululizo walikuwa wakilazimika kukosa shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria ili kuitikia wito wa Polisi kwa kuripoti jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Chadema wamekuwa wakitakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Kanda Maalum Dar es Salaam mara kwa mara tangu kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Maftah (22) mwezi uliopita.
Akwilina alipigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni na polisi waliokuwa wakijaribu kutawanya maandamanao ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wametoka kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni.

No comments:
Post a Comment