Tundu Lissu afunguka baada ya kufanyiwa oparesheni ya 19. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 15 March 2018

Tundu Lissu afunguka baada ya kufanyiwa oparesheni ya 19.

 
Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (Chadema)  Mhe Tundu Lissu amefunguka na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao kwake kufuatia oparesheni nyingine ya 19 ambayo amefanyiwa katika mguu wake.

Mhe Tundu Lissu Jana alifanikiwa kufanyiwa oparesheni hiyo katika mguu wake wa kulia na kuisha salama, madaktari waliamua kufanya oparesheni hiyo kufuatia kugundua moja ya mfupa wake ulikuwa ukichelewa kuunga na kudai kuwa kama wasingefanya upasuaji na kurekebisha mfupa huo ungeweza kuchelewa zaidi na kuja kuvunjika baadae.

"Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu" aliandika Tundu Lissu kupitia mtandao wake wa Instagram

Hata hivyo Watanzania mbalimbali wameendelea kumuombea Mhe  Tundu Lissu ili aweze kupona haraka na kurudia tena katika hali yake ya zamani ili aweze kurudi nyumbani Tanzania na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

Mhe Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi mnano Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma na kisha baadae kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo huku alifanyiwa oparesheni kadhaa katika mwili wake na baadae alikwenda nchino Beljium kwa matibabu zaidi ambapo jana amefanikiwa kufanyiwa oparesheni ya 19.

No comments:

Post a Comment

Popular