TRA kutoza kodi nyumba ambazo hazijakamilika. - KULUNZI FIKRA

Monday, 5 March 2018

TRA kutoza kodi nyumba ambazo hazijakamilika.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza kuwa, kuanzia mwaka ujao wa fedha 2018/19 kutakuwepo na mabadiliko katika kodi ya majengo ambapo, majengo ambayo hayajakamilika lakini yanatumiwa na watu yatatakiwa kulipiwa kodi. Hatua hiyo ni tofauti na mfumo wa sasa ambapo kodi hutozwa kwa majengo yaliyokamilika tu.

Hayo yalisemwa na Mwelimishaji Mkuu wa TRA, Rose Mhendeka katika mkutano na waandishi wa habari za blogu kuhusu kodi masuala ya kodi.

Ikiwa leo ni mwanzo wa wiki ya elimu kwa mlipakodi, Mhendeka alisema kuwa, awali kodi ya majengo ilikuwa katika sheria ndogo ndogo zinazosimamiwa na serikali za mitaa (by laws) lakini kwa sasa kodi hiyo ipo chini ya TRA na kwamba kuna uwiano katika viwango vinavyolipwa.

Alisema kuwa, nyumba ya kawaida inalipiwa TZS 10, 000 na ghorofa ni TZS 50,000 kwa sakafu (floor) lakini gharama inaweza
kubadilika kutokana na thamani ya nyumba yenyewe.

Aliongeza kuwa, awali watu hawakuwa wakilipa kodi kwa madai kuwa nyumba haijakamilika lakini unakuta wanakaa humo hadi miaka kumi, hivyo sasa wamebadili kigezo, na watakuwa wanaangalia nyumba kukaliwa na watu badala ya kukamilika.

Akiongezea jambo kwenye mada hiyo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alisema kwa sasa TRA inasimamia mapato yatokanayo na upangishwaji wa nyumba, hivyo ni jukumu la kila mhusika kulipa kodi hiyo ambayo ipo kisheria.

No comments:

Post a Comment

Popular