Taharuki yatokea Mahakama ya Kisutu. - KULUNZI FIKRA

Thursday 1 March 2018

Taharuki yatokea Mahakama ya Kisutu.

 
Kufuatia mvua kubwa inayonyesha jijini Dar es Salaam imesababisha hitilafu ya umeme katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Hifilafu hiyo imetokea katika chumba kimoja cha Mahakama na kusababisha mlipuko mkubwa ulioambatana na moshi. Inadaiwa chumba hicho kinatumiwa na Jaji Mashauri.

Mlipuko huo umewashtua watu wote waliokuwa mahakamani hapa ikiwemo Mahakimu na Maaskari na kusababisha watu kukimbia bila uwelekeo.

Baada ya hali hiyo Mahakama imewalazimu kuwatoa watu wote nje ya Mahakama na kusimamisha shughuli zote za Mahakama kwa muda.

Maaskari wanaendelea na juhudi za kuzima moto huo.

No comments:

Post a Comment

Popular