Serikali yalichukilia hatua gazeti lilohusika kumchafua Mange Kimambi. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 4 March 2018

Serikali yalichukilia hatua gazeti lilohusika kumchafua Mange Kimambi.

Serikali ya Tanzania kupitia kwa msemaji wake, Dkt Hassan Abbas amewaita wamiliki wa gazeti la Tanzanite ambalo linatoka mara moja kwa wiki (Jumatatu) baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na ukakasi wa habari zake.

Dkt Abbas ametoa taarifa hiyo ya wito kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “Nimepokea malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma katika toleo linaloonekana mtandaoni la gazeti la Tanzanite. Gazeti hili limesajiliwa kutoka kila Jumatatu. Hivyo tumewaita wahusika kesho baada ya kuona nakala halisi ili kupata maelezo yao.“.

Moja ya nakala ya gazeti hilo inayoonekana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyochapishwa Jumatatu ya wiki hii ina baadhi ya vichwa vya habari vinavyosomeka.

“Mbowe ameanza kuchanganyikiwa au ameamua kuudanganya umma?”, “Kila mwanaume ana tezi dume” “Hawa ndio Maadui wakubwa wa serikali ya Rais Magufuli (JPM)"
 

No comments:

Post a Comment

Popular