Mbunge wa Mtama (CCM) Mhe Nape Nnauye amefunguka na kuwataka Watanzania kutomlisha maneno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la kuongeza muda wa kuwa madarakani na kusema yeye alishasema hadharani hawezi kufanya hivyo.
Mhe Nape Nnauye amesema hayo siku moja baada ya kutoa kauli yake kuhusu baadhi ya viongozi wa Afrika ambao wamekuwa wakibadili Katiba za nchi zao ili kuendelea kubaki madarakani na kulifananisha suala hilo na ushetani na kuwataka vijana kupinga suala hilo.
"Hapa kwetu Rais John Pombe Magufuli alishasema hadharani kuwa 'hana mpango huo', kwahiyo tusimlishe maneno yeye aliapa kuilinda na kuitunza Katiba" alisema Mhe Nape Nnauye.
Mbali na hilo Mhe Nape Nnauye alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa hata Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Nkamia ambaye alitaka kupeleka hoja Bungeni ili ukomo wa uongozi uwe miaka saba badala ya miaka mitano ya sasa na kusema kuwa Mbunge huyo hoja hiyo alishaachana nayo muda mrefu.
"Nkamia mwenyewe alishaachana nayo nyie ndio mnaitamani kwa kuamsha marehemu, hoja ilishakufa kiherehere cha nini. Tamaa yeyote ya kuongeza muda bila kujali kafanya nani ni ushetani kwani unavuruga nchi" alisisitiza Mhe Nape Nnauye.

No comments:
Post a Comment