Nape Nnauye afunguka kuhusu Hussein Bashe. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 7 March 2018

Nape Nnauye afunguka kuhusu Hussein Bashe.

Mbunge wa Mtama (CCM) Mhe  Nape Nnauye amewataka Wabunge wa Tanzania bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kumuunga mkono Mbunge Hussein Bashe juu ya hoja yake binafsi aliyoiwasilisha kwa Katibu wa Bunge.

Mhe Nape ametoa kauli hiyo leo (Machi 07, 2018) baada ya kupita siku kadhaa tokea  Mbunge wa Nzega (CCM), Mhe  Hussein Bashe kudai amepeleka barua kwa Katibu wa Bunge na kupelekea kuibuka kwa baadhi ya wabubge wa upinzani kumpinga na kumuita mnafki kwa anachokitarajia kukifanya.

"Kazi ya Mbunge ni pamoja na kuwasemea wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hawana fursa ya kwenda wenyewe Bungeni. Tumuunge mkono Mhe Bashe bila kujali tofauti zetu za itikadi, dini au rangi", amesema Mhe  Nape.

Kwa upande mwingine, Mhe Nape amedai hoja binafsi ndani ya Bunge ni moja ya njia za kutafuta ukweli na suluhisho juu ya jambo fulani ambalo linatafutiwa ufumbuzi wake.

No comments:

Post a Comment

Popular