Waziri wa Mambo ya ndani, Dkt Mwigulu Nchemba amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.
Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dkt Mwigulu Nchemba amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.
"Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini kuna watu wengine hawaoni haya ila wao ni kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu," amesema Dkt Mwigulu Nchemba.
Pia Dkt Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.
Mbali na hayo Dkt Mwigulu Nchemba ameongeza kwamba majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.
"Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita," alieleza Dkt Mwigulu Nchemba.

No comments:
Post a Comment