Mo Ibrahim alivyojutia Benchi. - KULUNZI FIKRA

Saturday 3 March 2018

Mo Ibrahim alivyojutia Benchi.

Kaimu  Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’, amesema kiungo wa timu hiyo Mohamed Ibrahim ‘Mo Ibrahim’ amemwambia kuwa yupo tayari kubadili mwenendo wake klabuni hapo.

Hivi karibuni Kocha wa Simba, Pierre Lechantre, alisema mchezaji huyo amekuwa siyo ‘profesheno’, na anaomba udhuru mara nyingi kuliko wenzake jambo ambalo siyo sahihi, hivyo anatakiwa kubadilika.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana, Try Again alisema hata yeye jambo hilo lilimuumiza na kuamua kumuita mchezaji huyo ili kufahamu tatizo lake.

“Nilisikia kutoka kambini kuhusu utovu wa nidhamu wa Mo Ibrahim, na niliamua kumuita na kuzungumza naye baada ya kocha kuwa ameshasema.

“Nilimuuliza kama ana tatizo akanijibu kuwa hana tatizo lolote, nikamuuliza kwa nini hachangamki na analaumiwa na kocha akasema atabadilika.

“Aliposema atabadilika nilifurahia kwa kuwa huyu ni mchezaji mahiri sana kwenye timu yetu, hivyo nilimuambia aniandikie kwa barua kuwa atabadilika naye akafanya hivyo.

“Naamini kuwa sasa atakuwa amebadilika na ataendelea na programu za klabu kama zinavyotaka kwa kuwa amekiri mwenyewe nasi tutazungumza na kocha kumweleza tulipofikia,” alisema rais huyo.

No comments:

Post a Comment

Popular