Mnyeti aagiza Jeshi la polisi kumpa ulinzi Diwani wa chadema aliyejiuzulu. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 15 March 2018

Mnyeti aagiza Jeshi la polisi kumpa ulinzi Diwani wa chadema aliyejiuzulu.

 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, ametaka Diwani wa Kata ya Masakta , Marco Martini Kia (CHADEMA) amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM.

Apatiwe ulinzi wa kutosha.

Akizungumza mara baada ya diwani huyo kutangaza kujiuzulu na kuamua kurudisha kadi ya Chadema Mnyeti amesema anamkaribisha kwenye chama na kuwataka viongozi na wanachama wengine wajiunge na CCM.

Mnyeti amemwagiza Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo, kumpa ulinzi wa kutosha Kia, baada ya baadhi ya watu kumtishia maisha.

"OCD nakuagiza umpe ulinzi wa kutosha sitaki kusikia hata anaishi kwa wasiwasi baada ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa hiyari yake mwenyewe," amesema Mnyeti.

Wengine waliojiuzulu mwezi uliopita ni diwani wa kata ya Bagara Mjini Babati, Nicodemus Tlaghasi na diwani wa Hayderer wilayani Mbulu, Justin Masuja wa Chadema na Mathayo Semhenda wa kata ya Gehandu, Hanang kwa tiketi ya ACT- Wazalendo

Akizungumza Jana  Machi 15 mara baada ya kujiuzulu nafasi hiyo mbele Mnyeti, Kia amesema ameachia nafasi hiyo kutokana na kuunga mkono utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Mathew Darema amesema Kia ni kijana mchapakazi ila upande aliokuwapo ndiyo ulikuwa tatizo.

No comments:

Post a Comment

Popular