Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe amempa wakati mgumu Rais kufuatia ombi lake la kutaka wananchi ambao wamevamia msitu wa Mvomero kuachwa waendelee na maisha yao jambo ambalo Rais Magufuli amesema ni kinyume na sheria za nchi.
Rais Magufuli amesema kuwa anatambua ombi hilo la Mkuu wa Mkoa huyo limekuja baada ya kuona aliwaruhusu waendelea na maisha yao na kutofukuzwa watu waliovamia ardhi ya Wizara ya Elimu, wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo.
"Sasa ule msitu ambao upo karibu na Mvomero pale kumbe nao umeshavamiwa na viongozi wangu mpo mpaka zimefika nyumba elfu moja na kitu leo mnaniambia nifute ili kusudi hao watu waendelee kuishi hapo", alisema Rais Magufuli.
"Unajua inaumiza kweli na ombi hili nimeletewa kwa sababu niliwaruhusu watu wa Kahama kukaa kwenye maeneo yao sasa wanataka kuichukulia hii kama desturi lakini suala la Kahama lilikuwa tofauti na suala la hapa, ndiyo maana napata kigugumizi kuvunja sheria ambayo nimeapa kuilinda lakini Mkuu wa Mkoa ameliomba nitalibebe na kulifanyia kazi" alisema Magufuli
Aidha Rais Magufuli alitoa onyo kuwa jambo hilo sasa lisije kuwa mazoea watu kuvunja sheria kwa makusudi halafu wategemee kutumia kauli ya Rais kupata uhalali wa jambo hilo na kusema kama watu wakikata mapori yote nchi itakuwa jangwa.

No comments:
Post a Comment