Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi kutokana kusumbuliwa na maradhi ambayo hayajawekwa wazi.
Habari za uhakika zilizoifikia kulunzifikra blog Leo Machi 5, 2018, zinasema jana alipofikishwa katika hospitali hiyo saa mbili usiku na madaktari walimwekea mashine ya kumsaidia kupumua.
Taarifa za kulazwa kwa Mwenyekiti huyo ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai zilianza kuzagaa leo baada ya watu kumuona hospitalini hapo.
Katibu wa Chadema mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alipoulizwa juu ya kulazwa kwa kiongozi huyo alionekana kusita kuzungumza na kuhoji ni nani aliyetoa taarifa hizo.
Hata hivyo amesema, "Ni kweli jana aliugua ghafla na kupelekwa KCMC na madaktari walilazimika kumwekea Oksijeni ili ku stabilize (kudhibiti) afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni baada ya afya yake kuimarika.”
Lema alikataa kuingia kwa undani ugonjwa unaomsumbua kiongozi huyo akisema suala hilo ni siri ya mgonjwa na daktari wake zaidi ya kufafanua tu kuwa alipelekwa hospitalini hapo jana.
Habari zaidi zilizopatikana zilieleza kuwa asubuhi hii madaktari bingwa wa hospitali hiyo walikuwa wakimchukua vipimo ili kubaini maradhi yanayomsumbua.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vicent Mashinji na viongozi wengine wa chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi leo asubuhi Machi 5, 2018.
Februari 27, 2018 viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Mhe Freeman Mbowe ambaye leo hayupo kwa maelezo kuwa ni mgonjwa, walifika kituoni hapo na kuhojiwa kwa takribani saa tano, kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena leo.
Viongozi hao wakiongozwa na Dkt Mashinji ambaye Februari 27, 2018 hakufika kuhojiwa kutokana na kuwa nje ya nchi, mpaka saa 2:15 asubuhi walikuwa wamewasili wote kituoni hapo.
Mbali na Mashinji, viongozi wengine waliofika kituoni ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Pia, wamo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee; Mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa BAWACHA.
Viongozi hao wameambatana na wakili Frederick Kihwelo na Alex Massaba pamoja na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.
Massaba ameieleza kulunzifikra blog kuwa Mbowe hatoweza kufika kwa kuwa ni mgonjwa.
Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.
Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.
Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.

No comments:
Post a Comment