Kitabu cha maajabu ya Rais Magufuli ndani ya miaka Miwili. - KULUNZI FIKRA

Thursday 1 March 2018

Kitabu cha maajabu ya Rais Magufuli ndani ya miaka Miwili.

Kitabu cha Maajabu ya Rais John Pombe Joseph Magufuli , Kilichozinduliwa Jijini Dar es Salaam Na Waziri Wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo , Dk Harrison George Mwakyembe . Kimekuwa Ni Gumzo Nchini Na Jumuiya Ya Afrika Mashariki Nzima.

Akiongea Mratibu Mkuu Wa ' KITABU ' Ndgu Edward Stephano Haule Amesema Kitabu Hicho Ni Zao la Kitafiti na Kisera Kutoka Kampuni Ya Kizawa Ya NURU YA TAIFA PROJECT ya Nchini Tanzania Inayoongozwa na Vijana wa Kizarendo  Tanzania , Ambao Wapo wa Nne.

Akizungumza Mwandishi Mkuu wa 'KITABU' Ndgu Gadiel Joseph alisema haya alipozungumza na mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo alisema hicho kimechambua mambo mbalimbali ambayo Rais Magufuli ameyafanya ndani ya miaka miwili ya uongozi wake.

Alisema kwa muda aliokuwepo madarakani , Rais Magufuli amefanya mambo makubwa , ambayo ukilinganisha na utekelezaji huo ilitakiwa kufanyika kwa zaidi ya miaka 10.

Kitabu kinapatikana Vitabu Media Technologies Shop , Kariakoo ,  Congo / Amani , Mliman City , Irine   Stational Mwenge Bus Stand.

No comments:

Post a Comment

Popular