Beki wa kulia wa Yanga aliye kwenye kiwango cha hali ya juu kwa sasa, Hassan Kessy, ameibuka na kuweka wazi kuwa hawatafanya makosa mbele ya wapinzani wao, Township Rollers katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa kuhakikisha kwamba wanashinda kwenye mchezo wao wa hapa nyumbani.
Yanga wanaofundishwa na kocha George Lwandamina, kesho Jumanne watakuwa wenyeji wa Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na kulunzifikra blog, Kessy amesema kwamba wana uhakika wa kufanya vizuri katika mchezo huo kutokana na kufahamu umuhimu wa mchezo wa nyumbani sambamba na mbinu ambazo wamekuwa wakipewa na kocha wao, Lwandamina.
“Sote tunafahamu kwamba mchezo huu wa hapa nyumbani una umuhimu gani, hivyo tunajipanga kuhakikisha kwamba tunafanya tuwezavyo kwa ajili ya kushinda kwa ajili ya kujiwekea nafasi ya kutinga katika hatua inayofuata huko mbele, ni wazi kwamba tuna asilimia (kubwa) ya kushinda japo tunajua kwamba tutakutana na upinzani,” alisema Kessy.

No comments:
Post a Comment