Hofu yatanda ndani ya Klabu ya Yanga. - KULUNZI FIKRA

Monday, 5 March 2018

Hofu yatanda ndani ya Klabu ya Yanga.

Klabu ya Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga imeingiwa na hofu kuelekea mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana na kudai timu hiyo sio ya kuibeza kama baadhi ya watu wanavyofikilia.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa wanajangwani Charles Boniface Mkwasa leo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mtanange huo unaotarajiwa kuchezwa kesho (Machi 06, 2018) katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

"Hii timu siyo ya kuibeza ni timu ambayo inauwezo kiuchumi, nzuri na hata ukiangalia katika 'table' utaiona inaongoza kwenye ligi ya kwao Botswana. Kiukweli hii sio timu ya kuifanyia masihara", amesema Mkwasa.

Pamoja na hayo, Mkwasa ameendelea kwa kusema "nashukuru pia kusikia wachezaji wote wale waliokuwa majeruhi asilimia kubwa wamerejea katika hali zao na wamefanya mazoezi na wenzao kwa muda mrefu sasa. Tunamtegemea mwalimu na utaratibu wake wa mchezo atawachezesha wachezaji gani. Hii ni mechi kubwa yenye ushindani na mechi ambayo mshindi anakwenda katika hatua za makundi".

Mchezo wa kwanza kati ya Yanga na Township Rollers FC unatarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na kati na baada ya wiki moja timu ya Yanga itaradhimika kusafiri kwenda nchini Botswana  kwa ajili ya mechi ya marudiano.

No comments:

Post a Comment

Popular