Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu kwa kugombea Urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.
Mhe Lissu, ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo.
Kwa mujibu wa sheria mpya, Mhe Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote cha siasa, kuongoza chama hicho.
Katika kinyang’anyiro hicho, Fatma Karume atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi huku nafasi ya umakamu wa rais ikiwa na mgombea pekee, Rugemeleza Nshalla na Mweka Hazina akiwa Sadock Magai.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dkt Kibuta Ongwamuhana, uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.
Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma Karume ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kariba inayofanana na Mhe Lissu.
“Fatma Karume atashinda kwa sababu anapenda mtu mwenye ‘tension’ na ni mtu mwenye kujiamini anaweza akaitetemesha serikali na wanasheria wanapenda hivyo,” amesema mawakili wa kujitegemea ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Wakili mwingine alisema ingawa sheria hiyo inamkataza Mhe Lissu kugombea ambapo walipanga kumchagua tena mwaka huu lakini Fatma Karume anaweza kuziba pengo la Lissu.

No comments:
Post a Comment