Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema alikosea takwimu za deni la Taifa alizozitamka alipokuwa akikabidhi ripoti yake ya ukaguzi kwa Rais John Magufuli, mwanzoni mwa wiki.
Katika makabidhiano hayo, CAG alitahadharisha kwamba deni hilo lililofika Sh46 trilioni kutoka Sh41 trilioni kwa mwaka 2015/2016 sawa na ongezeko la asilimi 12 linatia wasiwasi na Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa huo.
Kwenye hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini hapa, CAG amesema: “Ukuaji wa deni ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka, tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) si mbaya lakini ikifika asilimia 76 nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie namna gani tunaweza ku-control (kudhibiti) ukuaji wa deni hilo.”
Licha ya kukosea huko tofauti na taarifa iliyomo kwenye ripoti yake, Rais Magufuli alimtoa wasiwasi akisema nchi inakopa na kuzitumia fedha hizo kutekeleza miradi ya maendeleo.
Baada ya kubaini alichokizungumza, leo Alhamisi Machi 29, 2018 Profesa Assad arekebisha kauli yake kuhusu mwenendo wa ukuaji wa deni la Taifa.
“Taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa deni la Taifa, hadi Juni 30, 2017 lilikuwa Sh46 trilioni. Katika deni hilo, Sh13.34 trilioni sawa na asilimia 29 ni deni la ndani na Sh32.75 trilioni sawa na asilimia 71 la nje. Deni hilo lote ni sawa na asilimia 31 ya Pato la Taifa (GDP) ambalo bado ni himilivu.”
CAG alikabidhi nakala ya ripoti yake kwa Rais katika tukio lililorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) huku akikumbusha kwamba ilipaswa kuwa siri kwa umma hadi itakapowasilishwa bungeni kabla ya Aprili 12 kwenye Bunge la Bajeti linalotarajia kuanza vikao vyake wiki ijayo.
Profesa huyo amesisitiza kwamba kilichokosewa ni matamshi yake lakini ripoti nzima iko vizuri na itakuwa wazi kwa ajili ya umma kufahamu kwa kila kitu kilichomo.

No comments:
Post a Comment