Baraza la Mawaziri waridhia kumuondoa Rais katika nafasi Yake. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 10 March 2018

Baraza la Mawaziri waridhia kumuondoa Rais katika nafasi Yake.

 
Katika kipindi ambacho Mauritius inajiandaa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, serikali imeamua kuzindua taratibu za kumshtaki bungeni ili kumfukuza Rais wa Jamhuri, Ameenah Gurib-Fakim.

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri ambao mwenyekiti alikuwa Waziri Mkuu Pravind Jugnauth mchana wa Alhamisi Machi 8, 2018.

Imeripotiwa kwamba mawaziri wa serikali walikubaliana kuwa rais huyo wa kwanza wa kike nchini atastahili kuondoka madarakani baada ya kuhusishwa katika kashfa ya matumizi ya fedha.

Gazeti maarufu la Express wiki iliyopita liliripoti kwamba Fakim alitumia mamia kwa maelfu ya rupia kwa manunuzi binafsi, kwa kutumia kadi ya mkopo ya Platinum iliyotolewa na shirika lisilo la serikali, la Planet Earth Institute (PEI).

Shirika la PEI linamilikiwa na Įlvaro Sobrinho, mfanyabiashara mwenye utata wa Angola ambaye mwanzoni aliwahi kufanya kazi na rais kutoa ofa ya masomo kwa wanafunzi wa Mauritius.

Rais awali alihoji uhalali wa ripoti za vyombo vya habari, lakini baadaye alidai amerejesha fedha zote zilizotumiwa na kadi ya mkopo. Rais, ambaye ni mwanasayansi maarufu, aliiambia Radio Plus kwamba hatajiuzulu.

"Sitajiuzulu. Waache waanzishe mashtaka yao. Nitaangalia baadaye ikiwa nina hatia. Tangu mwaka wa 2017, nimekwisha kurejesha fedha zote. "

Bunge linatarajiwa kuitwa wiki ijayo, baada ya sherehe ya Siku ya Uhuru Machi 12, na hoja itawasilishwa chini ya kifungu cha 30 (1) cha Katiba na ndiyo itakuwa agenda.

Chini ya kifungu cha 30 (1), Rais (au Makamu wa Rais) anaweza kuondolewa tu ikiwa...

(a) ukiukaji wa katiba au tendo lolote kubwa la uovu au

(b) kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi zake iwezekanavyo kutokana na udhaifu wa akili au mwili au kwa sababu nyingine yoyote.

Ili mchakato uanzishwe, Waziri Mkuu atapaswa kuwasilisha hoja bungeni kwamba mazingira ambayo yanahitaji kuondolewa kwa Rais au Makamu wa Rais yachunguzwe na mahakama.

Hoja hiyo lazima pia ifafanue kipekee mazingira ya kuondolewa kwa Rais yanahitajika kuungwa mkono na kura ambazo hazipungui theluthi mbili ya wabunge wote.

No comments:

Post a Comment

Popular