Zitto kabwe ataka maridhiano ya kitaifa kuhusu usalama wa nchi. - KULUNZI FIKRA

Saturday 24 February 2018

Zitto kabwe ataka maridhiano ya kitaifa kuhusu usalama wa nchi.

 
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mhe  Zitto Kabwe ametaka uitishwe mkutano wa kitaifa wa maridhiano ili kujadili hali ya kisiasa na usalama nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Jumamosi, Februari 24, 2018 jijini Arusha,  Mhe Zitto  Kabwe amesema katika mkutano huo zijadiliwe changamoto zote za kisiasa na kukubaliana kanuni za demokrasia ya vyama vingi.

"Hii ni kutokana na dhahiri kuwa mfumo wa vyama vingi nchini upo hatarini zaidi kuliko wakati wowote,” amesema Mhe  Zitto Kabwe.

Amesema mkutano huo unatakiwa kuwashirikisha pia viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji.

Amebainisha kuwa hali ya kisiasa sasa si ya kuwaachia wanasiasa pekee kwa kuwa pia inahusu uhai wa watu na wengine ambao hata hawajihusishi na siasa.

Mhe Zitto Kabwe yupo mkoani hapa kutembelea kata ambazo zina madiwani wa chama hicho na kuzungumza na wajumbe wa kamati za maendeleo za kata hizo.

No comments:

Post a Comment

Popular