Waziri wa Elimu abaini madudu chuo kikuu cha Kampala. - KULUNZI FIKRA

Tuesday 20 February 2018

Waziri wa Elimu abaini madudu chuo kikuu cha Kampala.

 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya ziara Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), kubaini baadhi ya walimu kuishi nchini bila vibali.

Katika ziara hiyo iliyofanyika leo Februari 20, 2018 Profesa Ndalichako ameambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala, mkuu wa Ithibati na Udhibiti Ubora wa Vyuo, Dkt Valerian Damian na maofisa mbalimbali kutoka idara ya uhamiaji na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Profesa Ndalichako amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwamo walimu wa chuo hicho kuajiriwa sehemu zaidi ya moja na kuishi nchini bila vibali.

"Wapo walioingia nchini kama wanafunzi lakini baada ya muda wakaajiriwa kama wafanyakazi, hii kwa sheria za nchi haikubaliki,” amesema Profesa Ndalichako.

No comments:

Post a Comment

Popular