Viongozi wa chadema watinga Tume ya Uchaguzi. - KULUNZI FIKRA

Thursday 15 February 2018

Viongozi wa chadema watinga Tume ya Uchaguzi.

 
Mwenyekiti wa Taifa wa (Chadema) Mhe  Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda ofisi ya NEC, kushinikiza wapewe viapo vya mawakala wao ambavyo mpaka sasa hawajapewa huku wakidai mawakala wa CCM wameshapewa.

Msafara huo wa viongozi hao ulipofika ofisi hizo kwa lengo la kukutana na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ramadhan Kairima waligonga mwamba baada ya watumishi wa NEC kudai kuwa Mkurugenzi huyo hayupo ofisini, viongozi hao waligoma kuondoka katika ofisi hiyo mpaka baadae Mbowe alipopata nafasi ya kwenda kuonana na Mkurugenzi huyo na kukubaliana.

Zifuatazao zilikuwa kauli za viongozi hao wakiwa kwenye ofisi hiyo ya NEC
Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee "Mnadhani tumekuja kunywa soda hapa sisi tumeacha shughuli muhimu kuliko hata nyinyi mnaokula ugali hapa, wewe tuma mtu aende pale amcheki Mkurugenzi ilo ndiyo jambo la mbolea ila hapa hatutoki, piga simu mtume mtu aulize kama Mkurugenzi yuko pale tunagawa timu wengine wanakwenda wengine tunabaki hapa"

Kwa upande wa Mhe John  Heche alikuwa na haya ya kusema "Kailima huyu kwenye Uchaguzi Mkuu nimempigia simu huyu madiwani wameondolewa nje ya utaratibu akarudisha leo kuongea na sisi moja kwa moja anashindwa nini? Na simu hapokei pia hata tulikuwa hatuna haja ya kuja hapa tunapiga simu hapokei, sisi tunamkutano jioni turuhusu tuingie tuonane naye twende kwenye mkutano, nyinyi mshaanza kusema tumevamia ofisi zenu kwa nguvu"

Mbali na huyo Mbunge wa Bunda mjini Mhe  Ester Bulaya naye alifunguka na kusema kuwa tayari mawakala wa Chama Cha Mapinduzi "CCM viapo wameshapewa wengine hamtaki kuwapa kama mnawaogopa watu mnaowagopa wa nini, sisi tusishiriki uchaguzi nyinyi mtapata faida gani"

Aidha Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa naye alihoji  "Au ndugu zetu mmeshapanga kutangaza matokeo mnavyotaka nyinyi"

Baada ya vuta vutana hiyo ya maneno baadaye Mhe  Mbowe aliweza kuingia ndani na alipotoka alikuwa na haya ya kusema kwa viongozi wengine wa Chadema waliofika hapo

"Nimemwambia kwamba sisi tumekuja kwa sababu hapokei simu zetu na maandishi yetu hayajibiwa kwa wakati na uchaguzi umekaribia na kuna mambo chungu nzima ya kurekebishwa kabla ya uchaguzi kwa hiyo tumekubaliana kwamba yeye naye lazima aitishe kikao chake na Tume ya Uchaguzi tukubaliane nao malalamiko gani ambayo tunayo halafu tupate muafaka kisha baadaye mchana awe amefanya mawasiliano", alisema Mhe Mbowe.

"Kama tutakutana tena mchana kuelekea jioni ili ratiba zingine ziendelee kwa hiyo mimi nimeridhika na hilo sioni kama kuna tatizo kwa hiyo cha msingi Waheshimu ninataka watu watatu wanne tukae sehemu tujadili mambo yetu halafu tumpigie simu maana anasubiri simu yetu jambo hilo", alisitiza Mhe Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Popular