Tundu Lissu afunguka mengi juu ya Kifungo cha Sugu. - KULUNZI FIKRA

Monday 26 February 2018

Tundu Lissu afunguka mengi juu ya Kifungo cha Sugu.

 
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu amefunguka kuhusu adhabu ya kifungo cha miezi mitano kwa Mbunge wa Mbeya Mjini na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.

Mhe Tundu Lissu kwanza alianza kwa kutoa pole kwa yaliyowakuta viongozi hao wa Chadema lakini baadaye ametoa ufafanuzi kuhusu hukumu hiyo na kudai hukumu hiyo siyo mwisho wa mjadala mahakamani. 

"Bado kuna fursa, na haki ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal. Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past. Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu", alisema Mhe Tundu Lissu.

"Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya 'utovu wa uaminifu.' Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu", alisema Mhe Tundu Lissu.


"Pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana. Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani", alisema Mhe Tundu Lissu.

"On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They'll come out even bigger and stronger than when they went in" alisema Mhe Tundu Lissu.

No comments:

Post a Comment

Popular