Mamlaka ya Mapato (TRA) imekamata na kutaifisha vifaranga vya kuku 5,000 vilivyokuwa vikiingizwa juzi nchini kupitia mpaka wa Kenya katika mji wa Namanga mkoani Arusha na sasa vitateketezwa.
Vifaranga hivyo ni sehemu ya bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na TRA zikiingizwa nchini kwa magendo, ikiwa ni pamoja na mayai kasha 416, tani moja ya sukari na chumvi, majani ya chai mifuko 18 na mirungi kilo 16.
Hii ni mara ya pili katika miezi minne kwa TRA kukamata vifaranga vya kuku mpakani hapo baada ya 6,400 vilivyoingizwa kutoka Kenya kupitia mpaka wa Namanga kuteketezwa kwa kuchomwa moto Oktoba, mwaka jana na mamlaka za wilayani Longido.
Akizungumza baada ya kukamata bidhaa hizo, Meneja Msaidizi wa Forodha mkoani hapa, Edwin Iwato, alisema vifaranga hivyo ni mali ya Andrew Lymo.
"Tumewakamata wafanyabiashara watatu ambao ni Joseph Sekino akiwa amepakia tani moja ya sukari na chumvi na majani ya chai mifuko 18 kwenye gari T 785 AWV, Innocent Minja akiwa na mayai kasha 416 na mirungi kilo 16 kwenye gari T 443 CQU na Andrew Lymo akiwa na vifaranga vya kuku 5,000 kwenye gari T441 DHW, wote wakitokea nchini Kenya kuja mkoani Arusha", alisema Iwato.
Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, alisema bidhaa zote haramu zilizokamatwa, zikiwemo vifaranga, zitateketezwa kwa mujibu wa sheria.
Alisema zile zinazofaa kwa matumizi ya binadamu zitagawiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zenye uhitaji kwa mujibu na taratibu zilizowekwa na TRA.
Uteketezaji wa vifaranga 6,400 kwa kuvichoma moto uliibua malalamiko kutoka kwa jamii na watetezi wa haki za wanyama Novemba mwaka jana.

No comments:
Post a Comment