Zikiwa zimebakia takribani siku 9 kuelekea marudio ya uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni hali imekuwa tofauti kwa wagombea Salum Mwalimu pamoja na Maulid Mtulia kwa kutoleana maneno ya kejeli pindi walipokutana uso kwa uso.
Wakizungumza katika nyakati tofauti tofauti leo (Alhamisi) kwenye kituo kimoja cha Radio wagombea hao ambapo ndio mara ya kwanza kukutana pamoja kuongelea masuala ya maendeleo katika jimbo hilo ambalo kila mmoja analiwinda kwa namna yake ili aweze kuwatumikia wananchi hao katika siku za usoni kutoka sasa.
Salum Mwalimu amesema sio kweli kwamba ukiwa katika chama tawala kama anavyojitapa mgombea mwenzake kuwa ndio chanzo cha kupelekea maendeleo wananchi kwa madai maendeleo yanapangwa ndani ya Bunge nasio penginepo.
"Mimi niseme tu maendeleo yanapangwa bungeni na hakuna mtu mwingine anaweza kupanga nje ya Bunge. Unapojadili bungeni mule hayapangwi kwa vyama, kwamba wewe ni chama X unapewa kikubwa na mwingine Y amepewe kidogo hapana. Keki ya taifa hii tunayoiita ni ndogo ndio maana uwezo wa kuhimili bajeti yetu ya maendeleo kwa mwaka haitoshelezi tunalazimika kuomba misaada na kulazimika kukomba sehemu nyingine mbalimbali", amesema Salum Mwalimu.
Kutokana na hayo, Maulid Mtulia amemjibu mwenzake kwa kudai hajui alisemalo kwa kuwa hajawahi kuwa hata Mbunge hivyo hapaswi kusema lolote juu ya hilo.
"Kwanza kaka yangu hajawahi kuwa Mbunge kwa hiyo anachokisema hakijui kama ninavyokijua mimi, mwenzake nimekaa miaka miwili na yeye anasema anataka kwenda kukalia kiti changu kwa hiyo kwa maana nyingine achunge maneno yake asiseme asiyoyajua. Mimi ndio napaswa kusema", amesema Mtulia.

No comments:
Post a Comment