Sababu zilizofaya Jacob Zuma Kuachia ngazi. - KULUNZI FIKRA

Thursday 15 February 2018

Sababu zilizofaya Jacob Zuma Kuachia ngazi.

Jacob Gedleyihlekisa Zuma ni jina ambalo limekuwa common sana kwa Afrika tangu mwanaume huyu mwenye asili ya kabila la Zulu aingie madarakni na kuwa Rais wa Afrika Kusini kupitia chama cha ANC.

Wakati akiingia madarakani Jacob Zuma alikuwa kiongozi mwenye kupendwa na watu, na hiyo ikiwa ni moja ya kigezo kikubwa kilichomuweka madarakani kwenye uchaguzi mkuu wa Mei 2009, na kuanza kuiongoza nchi hiyo baada ya Thabo Mbeki kujiuzulu kutokana na kashfa za rushwa.

Taarifa kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba Jacob Zuma alikuwa akipendwa na watu kutokana na utu wake, kujishusha na kuishi kama mtu wa kawaida na kutodharau masikini, alikuwa mtu wa watu na waafrika Kusini wengi walimpenda Jacob Zuma.

Kabla ya kushika wadhifa mbali mbali ndani ya chama cha NAC na hatimaye kuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma wakati wa ujana wake alikuwa ni miongoni mwa vijana waliokuwa mstari wa mbele kupinga serikali ya ubaguzi wa rangi, na kumpelekea kufungwa jela miaka 10 kwenye gereza ambalo Nelson Mandela alifungwa na makaburu.

Katika maisha yake Jacob Zuma aliishi kwa kufuata pia misingi ya kabila lake la Zulu, ikiwemo kuwa na ndoa za mitala, na kuwa na jumla ya wake 6, mmoja alitalikiana naye, mmoja alijiua, na mpaka sasa ana jumla ya wake wanne.

Alipoingia madarakani Jacob Zuma alianza kuandamwa na kashfa mbali mbali kama za ngono, rushwa na ufujaji mali, kashfa ambazo alizikana na mpaka zingine kufikia hatua ya kupandishwa mahakamani.

Wakati akiwa kiongozi ndani ya chama cha ANC, Jacob Zuma alishawahi kushtakiwa kwa kumbaka rafiki wa familia mwenye maambukizi ya VVU, lakini alishinda keshi hiyo baada ya mahakama kumkuta hana hatia.

Angalia hapa orodha ya mashtaka ambayo yamepelekea Jacob Zuma kutoka madarakani kabla ya muda kuisha na bila kupenda.

2005: Alituhumiwa kwa rushwa ya mabilioni ya dola kwenye mkataba wa silaha wa mwaka 1999 madai ambayo yalitupiliwa mbali kabla hajawa rais mwaka 2009

2005: Aishitakiwa kwa kumb'aka rafiki wa familia na kufutiwa mashitaka mwaka 2006
2016: Mahakama iliamuru ashitakiwe kwa makosa 18 ya rushwa dhidi ya mkataba wa silaha ambao alikatia rufaa

2016: Mahakama iliamuru kuwa amekiuka kiapo chake kama raisi na kutumia fedha za serikali kuboresha makazi yake binafsi fedha ambazo alizilipa baadae

2017: Wakili wa serikali alisema ateua jaji kiongozi wa kamati ya kuchunguza iwapo ana uhusiano na familia tajiri ya Gupta ambaye ni rafiki yake mkubwa, madai ambayo ameyakanusha

Lakini licha ya hayo yote, Mnamo Februari 13, 2018, chama cha ANC mabacho tayari kilimvua madaraka ya kukiongoza chama hiko na kushikiliwa na Cyril Ramaphosa, kilimtaka Zuma ajiuzulu, Zuma alianza kwa kukubali na kuomba muda wa miezi mitatu hadi 6, lakini baadaye alisema haoni sababu ya kujiuzulu kwani hana kosa, na ndipo chama hiko kikafanya msisitizo wa kumn'goa madarakani na hatimaye, usikuwa Februari 14 Jacob Zuma alitangaza kujiuzulu urais wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular