Polepole afunguka mengi baada ya matokeo ya uchaguzi. - KULUNZI FIKRA

Sunday 18 February 2018

Polepole afunguka mengi baada ya matokeo ya uchaguzi.

katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM  Ndugu Humphrey Polepole, amesema chama cha Mapinduzi (CCM) kilijua kuwa kitashinda kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika.

Akizungumza na mwandishi wa kulunzifikra blog, Ndugu  Polepole amesema watu wameiamini CCM kwa sababu inawajibika kwao, hivyo ahlikuwa suala humu wao kupatra ushindi.

“Niwashukuru kwa kujitokeza, niwashukuru kwa kuwa watulivu, wananchi wengi walionyesha kiu yao ya kupata wawakilishi ambao watwachagua wenyewe, wengi wao walieleza wanapenda kuona kazi nzuri ambayo Rais anaifanya inafanyika katika majimbo hayo", amesema Ndugu Polepole.

"Matokeo yameeleza sauti ya watanzania katika maeneo haya, CCM kwa mara nyingine tumeshinda kwa kishindo, sisi tulijua kuwa tutashinda, kwa sababu ya kazi nzuri ambayo serikali ya CCM ilikuwa ikiifanya”, amesema Ndugu  PolePole.

Licha ya hayo  Ndugu Pole pole amesema kuwa kitendo cha vurugu kilichotokea pia walijua kuwa wapinzani wataleta vurugu, kwani kufanya vurugu ndio kawaida yao.

No comments:

Post a Comment

Popular