Naibu spika azidi kumubana Peter Msigwa. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 10 February 2018

Naibu spika azidi kumubana Peter Msigwa.

 
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Mwansasu amempeleka Mbunge wa Iringa  Mhe  Peter Msigwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (E-Immigration).

Naibu spika Tulia Ackson amesema hayo baada ya Mhe  Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika katika mradi huo chini ya Serikali ambayo inajipambanua kupambana na ufisadi. Kufuatia kauli hiyo ndipo hapo Naibu Spika aliagiza Mbunge huyo kwenda kutoa taarifa hizo kwa Kamati ya maadili. 

"Mhe  Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi" alisema  Naibu spika Tulia Ackson.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt  John Pombe Magufuli  Januari 31, 2018  alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Popular