Mwigulu Nchemba atoa onyo kwa Chadema kuhusu tukio la Tundu Lissu. - KULUNZI FIKRA

Wednesday 14 February 2018

Mwigulu Nchemba atoa onyo kwa Chadema kuhusu tukio la Tundu Lissu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe  Mwigulu Nchemba amefunguka na kuweka wazi kuwa baadhi ya wanasiasa wanaohubiri sakata la Lissu kupigwa risasi wanafanya siasa kwani ukweli ni kwamba bila serikali kiongozi huyo angekuwa amepoteza maisha.

Mhe Mwigulu Nchemba amesema hayo leo Februari 14, 2018 akiwa Singida na kudai kuwa bila jitihada za serikali huenda Mbunge huyo wa Singida Mashariki Tundu Lissu angekuwa amepoteza maisha kufuatia shambulio la kupigwa risasi akiwa mjini Dodoma.

"Mhe Tundu Lissu aliposhambuliwa daktari aliyekwenda kuokoa maisha yake yaani huduma ya kwanza ile ambayo isingefanyika Lissu angepoteza maisha yake ilifanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ni mteule wa Rais, Katibu Mkuu alikwenda kuvaa joho kwa sababu yeye ndiye mtalaam aliyebobea ili aokoe maisha ya ndugu yetu, basi daktari yule pamoja na madaktri wengine ambao wao ndiyo Serikali wasingefanya huduma ya kwanza ile ya kuzuia damu kutoka ndugu yetu asingepona" alisisitiza Mhe  Mwigulu Nchemba. 

Mhe Mwigulu Nchemba aliendelea kuzungumza, "Hawa wanakuja wanaongea ongea juu ya Lissu hata hawatokei hapa Singida angekuwa mtu anayetokea Singida ilibidi aipongeze Serikali kwa kazi iliyofanya baada ya Lissu kushambuliwa"  alisisitiza Mhe Mwigulu Nchemba.

Mbali na hilo Mhe  Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kutotumia tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na kufanyia siasa.

No comments:

Post a Comment

Popular