Mchungaji Mwingira afurahia maamuzi ya Mahakama. - KULUNZI FIKRA

Monday 26 February 2018

Mchungaji Mwingira afurahia maamuzi ya Mahakama.

 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifukuzia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dkt William Morris raia wa Marekani dhidi ya mke wake Dkt Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira kwa garama.

Dkt William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo, akiomba, mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha DNA.Katika Maombi hayo Dk. Morris ambae ni mume wa (mdaiwa wa Pili, Philis Nyimbi) anaiomba Mahakama itoe amri ya mkewe Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA.

Lengo ni kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.Katika madai yake, Dkt Morris anadai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume( 9).

Mapema mahakamani hapo,akisoma hukumu hiyo leo February 26 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dkt Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonesha mahusiano ya kimapenzi kati ya Dkt Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa Dk. Morris ni matokeo ya mahusiano ya kimapenzi kati ya Dkt Phills na Mchungaji Mwingira.Hivyo mahakama imeifukuzia mbali kesi hiyo ya madai na kueleza mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.

"Si tu ameshindwa moja kwa moja lakini ameshindwa kiasi ambacho Mahakama hii inalazimika kutoa amri kuwa alipe garama walizotumia wadaiwa kwenye shauri hili" amesoma Hakimu Simba.Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo Wakili wa mdai, Respicius Ishengoma amesema hawajaridhika na uamuzi huo na watakata rufaa.

Hukumu hiyo iliyoandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini imesomwa leo nyakati za saa 8 mchana.Awali kwenye utetezi wa Dkt Phills Nyimbi aliieleza Mahakama hiyo hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.

No comments:

Post a Comment

Popular