Mbowe: Hukumu ya Sugu ilipangwa hoteini. - KULUNZI FIKRA

Tuesday 27 February 2018

Mbowe: Hukumu ya Sugu ilipangwa hoteini.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe Freeman Mbowe amedai kuwa hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi ‘SUGU’ ilipangwa hotelini siku 4  kabla ya mahakama kutoa hukumu.

Mhe Mbowe amesema kuwa suala hilo lilipangwa na hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala alilijua hilo kuwa Mhe  Sugu atafungwa huku akimtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala kuhusika.

“Hukumu ya Mhe Sugu ilifahamika na ilipangwa hotelini, kwamba Sugu anafungwa miezi mitano tulipata taarifa hizo siku 4 kabla. Na kwamba polisi walikusanywa mkoa mzima wa Mbeya, Mkoa mzima wa Songwe, watu wa usalama wa taifa wakajazwa Mbeya kukabiliana na presha ya wananchi ni jambo liliratibiwa", amesema Mhe Mbowe.

"Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anauhusika na anajua jambo hili, Amosi Makala,”amesema Mhe. Mbowe leo Jumanne kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za makao makuu Jijini Dar es salaam", amesema Mhe Mbowe.

Kwa upande mwingine Mhe Mbowe amesema kuwa Chadema hawaingilii maamuzi ya mahakama bali wanawasema baadhi ya watendaji wa mahakama wanaotumika kisiasa.

“Tunaiheshimu sana mahakama, Muhimili wa mahakama ndio muhimili ambao unasaidia wa Kuregulate nchi, lakini mahakimu mmoja mmoja wanapotumika ndio wanaichafua mahakama na wanalichafua taifa,“amesema Mhe  Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Popular