Mbowe amjia juu Musiba. - KULUNZI FIKRA

Tuesday 27 February 2018

Mbowe amjia juu Musiba.

 
Mwenyekiti  wa Chadema Taifa,  Mhe Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa kitendo cha Mkurugenzi wa kampuni ya CZI, Cyprian Musiba kumtaja yeye kati ya watu anaosema ni hatari kwa taifa ni mpango mkakati na kuwa mtu huyo ametumwa.

Mhe Mbowe amesema hayo leo Februari 27, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kabla ya kwenda kuripoti Makao Makuu ya jeshi la polisi ambapo walikuwa wanakwenda kuripoti.

"Majuzi amejitokeza mtu anaitwa Musiba na akanishambulia kwamba Chadema na Mbowe ni watu hatari na viongozi wangu kadhaa wametajwa pamoja viongozi wa vyama vingine na taasisi zingine, yule mtu akatoa shtuma za kipumbavu kabisaa, tena akizihusiha nchi ambazo ni washirika wetu wa maendeleo, yule bwana hakusema yeye yale maneno bali amelishwa yale maneno " alisema  Mhe Mbowe.

Mhe Mbowe aliendelea kusema kuwa mtu huyo alitumwa kusema vile ili kuliandaa taifa juu ya kuja kukamatwa kwao kutokana na tukio lililotokea Februari 16, 2018 ambalo lilipelekea kifo cha mwanafunzi mmoja na watu wengine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi, Mbowe anasema toka kutokea kwa tukio hilo kumekuwa na jitihada kubwa kuhakikisha viongozi hao wa Chadema wanahusishwa. 

"Ili kuliandaaa taifa na mazingira ya kuwakamata kina Mbowe, Heche, mtu yule anasema tunafundisha vijana zaidi ya mia nne Ujerumani namna ya kuleta vurugu nchini na akaenda mbele zaidi na kusema kuwa kijana Yericko Nyerere. Yericko Nyerere hajawahi kufundishwa na chama hiki na wala hajawahi kuwa mtendaji wa chama hiki bali ni Mtanzania mwenye mapenzi mema na Demokrasia na mwanachama wetu", alisema Mhe Mbowe.

"Sasa hawa wanaliandaa taifa na wanaandaaa katika style za kijinga ambazo zinafanya hata mahusiano yetu na mataifa makubwa nje yaingie kwenye doa na kuleta shida kwa mambo ambayo hayana maana hiyo yote ni katika kuuwa demokrasia katika nchi hii" alisisitiza Mbowe 

No comments:

Post a Comment

Popular