Mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Akwilina. - KULUNZI FIKRA

Thursday 22 February 2018

Mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Akwilina.

Mamia  ya wananchi na viongozi wa Serikali wapo kwenye viwanja vya Chuo Cha Usafirishaji (NIT), Dar es Salaam kuuaga mwili wa mwanafunzi wa chuo hicho aliyepoteza maisha kwa kupigwa risasi Februari 16, Kinondoni jijini humo.

Baada ya kuagwa, mwili wa msichana huyo, Akwilina Maftah (22) utasafirishwa kwenda Rombo , Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Viongozi kadhaa wa serikali wamejumuika na wananchi kumuaga Akwilina akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye, na Mkuu wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Mwili wa marehemu Akwilina umefikishwa kwenye viwanja vya NIT mchana huu ukitolewa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Popular